Moto Mkubwa Waikumbumba Hallywood, Haijawahi Kutokea Katika Historia – Video – Global Publishers



Moto mkubwa na wa kutisha umeibuka katika maeneo ya Hollywood Hills, Los Angeles, Marekani, na kusababisha taharuki kubwa. Maelfu ya wakazi wameamriwa kuondoka mara moja, huku wengine zaidi ya 100,000 wakihimizwa kuwa tayari kuhamishwa wakati wowote.


Moto huu, ambao ulianza kwa kasi siku ya Jumatano, Januari 9, saa 12 jioni kwa saa za Los Angeles, tayari umeathiri eneo la Runyon Canyon na kuteketeza zaidi ya ekari 20 pamoja na nyumba kadhaa, zikiwemo zile za kifahari.
Kwa mujibu wa taarifa, watu watano wamepoteza maisha hadi sasa kutokana na janga hili la moto. Zaidi ya majengo 1,000 yameripotiwa kuharibiwa kabisa, na maelfu ya wakazi wa Los Angeles wamesalia bila makazi, wakiwa wamepoteza kila kitu.

Moto huu, unaojulikana kama Sunset Fire, sasa umesambaa katika maeneo maarufu ya mastaa, ukiathiri vivutio kama Hollywood Walk of Fame, ukumbi wa sinema wa TLC Chinese Theatre, na eneo la burudani la Hollywood Bowl.











Related Posts