BALOZI WA JAPANI AMALIZA MUDA WAKE WA UWAKILISHI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amemuaga Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yasushi Misawa anayetarajia kumaliza muda wake wa uwakilishi Januari 17, 2025.

Mhe. Kombo ameishukuru Japan kwa kuwa miongoni mwa wadau wanaosaidia kufanikisha Miradi ya Maendeleo hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, biashara, afya, kilimo, nishati na elimu.

Aidha, ameeleza umuhimu wa kuongeza ushirikiano katika biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili kupitia maonesho ya Biashara huku akiwaalika kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yatakayofanyika mwezi Julai 2025.

Kwa upande wake Balozi Misawa ameishukuru Wizara kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake ya kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Japan kwa kipindi alichohudumu cha takribani miaka miwili na miezi saba hapa nchini.

Halikadhalika, Mhe. Waziri Kombo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kudumisha kazi nzuri aliyoifanya na itampatia ushirikiano wa kutosha Balozi mpya wa Japan atakayepangwa kuhudumu Tanzania.













Related Posts