Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Husna Sekiboko leo tarehe 10 January 2025 amekabidhi vifaa vya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UWT Mkoa wa Tanga vyenye thamani ya shiling million 5.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni TOFALI za kujenga nyumba yote, SIMENTI , MAWE , MCHANGA NA KOKOTO
Katika makabidhiano hayo Sekiboko ameipongeza Kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Mama Alshaimaa kwa kupata kiwanja vizuri ktk eneo zuri Jijini Tanga, na ameahidi kushirikiana kwa karibu na Uongozi wa UWT Mkoa katika ujenzi wa nyumba hiyo MPAKA IKAMILIKE.
Sekiboko amesema ametoa vifaa hivyo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo yaliyotelewa na Viongozi mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Rajab Abdulrahman pamoja na Mwenyekiti wa UWT Taifa ambaye pia ni (MCC) Mary Chatanda
Kwa upande wake Katibu wa UWT MKOA WA TANGA amesema Vifaa hivyo vitawasaidia katika kukamilisha nyumba hiyo ambayo wanajenga eneo la Mbungani kata ya Masiwani Jijini Tanga.
Kaimu Mwenyekiti wa UWT Mkoa Moza Shiling amesema amesema walishawahi kuwa na viongozi wengi lakini husna Sekiboko amefanya makubwa na haijawahi kutokea .
Salim Perembo Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Diwani wa Kata ya Majengo alisema uwt imepata kiongozi mwenye upendo na ambaye anawafundisha siasa.
Katibu wa Madiwani Jiji la Tanga Habiba Namalecha alisema wanajivunia kuwa na Husna Sekiboko na hawakufanya makosa kumchagua sababu anafanya mengi makubwa na yakuwaletea maendelea nadani ya chama na jumuiya.