WAWEKEZAJI Nchini Wahakikishiwa Usalama na Amani ili wa Mali zao ili waweze Kufanya Uwekezaji wenye tija kwa Maslahi mapana ya Taifa .
Akizungumza na Wanahabari Leo Januari 10,2025 Wakati wa Uzinduzi wa mradi Wa Nyumba za Kisasa (Milano Appartment) uliopo Masaki JijiniDaresSalaam,Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Hassan Suluhu Kwa Kuifungua nchi Kimataifa na Kuhakikisha hali ya Usalama wa Raia na nchi kwa ujumla.
“Mama Samia ameifungua nchi Kimataifa ambapo imekuwa shawishi Kwa wekezaji kuendelea Kuwekeza nchini Tanzania.”
Pia Kumbilamoto hivi punde watatoa taarifa kwa namna gani baadhi ya Viwanja na Maeneo yataweza Kukodishwa kwa ajili ya Uwekezaji kwa Jiji La Dar es Salaam ili kuruhusu Wawekezaji nchini Kufanya Biashara.
Hata hivyo ameongeza kuwa amefarijika Kwa kuona Wawekezaji Wazawa Kwa kuunga Mkono uwekezaji huo wa Makazi ya Kisasa (Appartment) akimtolea mfano Mwekezaji wa mradi huo Jedda Hassanabuba kwa kuthubutu .
Kwa Upande wake Muwekezaji katika Mradi huo wa Milano Jedda Hasabubaba amesema mradi huo kwa kushirikiana na wachina ni mradi ambao umekidhi mahitaji yote na ni sehemu sahihi kwa watu wote.
Hata hivyo amewataka Wasanii na Watu Maarufu Kufanya shughuli zao ndani ya Makazi yao kutokana na umaridadi na unadhifu wa Makazi hao.
“Miundombinu salama na inavutia kwa shughuli zote hivyo hata Wasanii kutengeneza Kazi zao katika ubora wa hali ya juu.”