Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Ignace Senga akipokea zawadi mbalimbali za ofisi ikiwa ni pamoja na kalenda ya mwaka 2025 kutoka kwa Meneja wa tawi la benki ya NMB wilaya ya Mbozi, Greyson John Komba akiwa ameambatana na Mdhibiti Ubora wa Tawi, Fausta Lusekelo , walipotembelea ofisi ya Kamanda Januari 10, 2025 kwa lengo la kutoa shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa Ushirikiano wanaopata unaowawezesha kuendelea kufanya shughuli zake kwa ufanisi ikiwemo na kumpa zawadi za mwanzo wa mwaka pamoja na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa elimu wanayoitoa kupitia makundi mbalimbali kwenye jami, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa kibiashara kati ya Jeshi la Polisi na benki ya NMB.