RAIS MSTAAFU DKT.KIKWETE ASHIRIKI MIKUTANO YA KUBORESHA KILIMO

RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika (Africa Food Prize Committee) na Mjumbe wa Bodi ya AGRA, anashiriki Mikutano mbalimbali kuhusu uboreshaji wa kilimo barani Afrika, kuelekea kupitishwa kwa Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 – 2035), Kampala, nchini Uganda.

Mikutano hii itafikia kilele kwa kupitishwa kwa Azimio la Kampala, na mkakati wa kihistoria wa miaka kumi na mpango kazi, ili kuimarisha utekelezaji wa Azimio la Malabo kuhusu Ukuaji wa Kasi wa Kilimo na Mabadiliko kwa Ustawi wa Pamoja na Maisha Bora, lililopitishwa mwaka 2014.

Related Posts