Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa majaji katika Mahakama ya rufani, wenyeviti wa Bodi na pia amempangia kituo cha kazi Balozi Moses Kisiluka.
Katika taarifa iliyotolewa katika ukurasa rasmi wa mawasiliano ya ikulu na Mkurugenzi wa mawasiliano Sharifa Nyanga, inaeleza kuwa uapisho majaji wa Mahakama ya rufani utafanyika katika tarehe iliyopangwa.