KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA UKIMWI YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA UKIMWI NJOMBE

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) imezitaka halmashauri, taasisi, na wadau mbalimbali wanaonufaika na mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini kutumia vyema fursa hizo. 

Imepongeza ushirikiano uliopo baina ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, ambacho kimeendelea kutoa mafunzo wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuongeza ufanisi wa kufuatilia na kusimamia maendeleo ya miradi ya serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 10, 2024, na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, na Uratibu, John Bosco Quman, wakati wa kufunga mafunzo ya uelewa kwa watumishi wa serikali ngazi ya halmashauri. 

Quman amehimiza washiriki kushiriki kikamilifu hatua zote tatu za mafunzo ili kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha amekipongeza Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Quman amesema chuo hicho kimefanya kazi nzuri katika kutoa mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini, bila malalamiko yoyote kuhusu utekelezaji wa mpango huo unaosimamiwa na serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Huria, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wafanyakazi wa serikali. Hadi sasa, mikoa yote nchini imefaidika na mafunzo hayo katika ngazi ya kwanza. 

Ameongeza kuwa washiriki 67 kutoka halmashauri mbalimbali wamepata maarifa ya kutafsiri miongozo, kusimamia utekelezaji wa miradi, na kuandaa miongozo inayosaidia kutatua changamoto za kijamii katika mafunzo yaliyotolewa Mkoani Morogoro .

Naye, Caroline Marila, mshiriki wa mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, amesema mafunzo hayo yataboresha utekelezaji wa miradi ya serikali na usimamizi wa rasilimali fedha, hivyo kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Mafunzo haya, yaliyoanzishwa na serikali kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, yalianza mwaka 2024 kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa umma katika kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi wa matumizi ya rasilimali.

Related Posts