Kinda la Yanga laingia kikosi bora

KINDA wa Yanga, Shaibu Mtita anayekipiga Wakiso Giants ya Uganda ameingia kwenye kikosi bora cha raundi ya 15 baada ya kufanya vizuri kwenye nusu ya msimu wa ligi ya nchi hiyo.

Mtita pamoja na Isaack Emmanuel ‘Mtengwa’ wapo Wakiso kwa mkopo wakitokea Yanga ya vijana U-20 ambako walifanya vizuri wakicheza baadhi ya mashindano, Mapinduzi Cup na Kombe la FA.

Kwa mujibu wa TUF UG orodha ya wachezaji 11 waliofanya vizuri mzunguko wa kwanza wa Ligi yumo Mtita kwenye eneo la beki wa kati.

Akiwa mchezaji pekee wa Wakiso aliyeingia kwenye orodha hiyo anadhihirisha uwezo mkubwa aliojaaliwa kwenye miguu yake na kichwani.

Timu hiyo imeonja ushindi mara mbili kati ya mechi 15, sare sita na kupoteza michezo saba ikikusanya pointi 12 huku ikisalia nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi.

Kwenye michezo 15, Mtita amecheza 13 kwa dakika 941.

Related Posts