BSL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USALAMA BARABARANI ZINGA

Afisa Utawala Kiwanda Cha Bagamoyo Sugar Limited Ibrahim Juma Mohammed  akimkabidhi  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Shaibu Ndemanga  (kulia) vikoti vya kuakisi mwanga 80 ambavyo vitatumiwa na Jeshi la Polisi Barabarani katika Kata ya Zinga makabidhiano hayo yamefanyika  leo  tarehe 13,Januari 2025.

Wanafunzi wa Shule mbalimbali  zilizopo Kata ya Zinga wakimsikiliza kwa makini Sgt.Otilia Ponera akiwapa  maelekezo ya kuhusu kuzingatia usalama wao wanapovuka barabara  hasa kwenye eneo la Pundamilia.

Na Khadija Kalili, Michuzi  Tv 

KIWANDA cha sukari Bagamoyo Sugar kilichopo Wilayani hapa leo Januari 13, 2025 wametoa  vifaa vya Usalama  barabarani ambavyo vitatumika katika kuongoza  na kupunguza ajali za barabarani  kwa wanafunzi na raia katika Kata ya Zinga.

 

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Afisa Utawala BSL,  Ibrahim  Juma Mohammed amesema kuwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja  viakisi mwanga 80 pamoja na vibao vya kuongoza magari kwenda na kusimama ikiwa ni katika kupunguza ajali za barabarani  ambazo imeelezwa kukithiri katika  eneo hiyo.

Mohammed amesema kuwa  vifaa hivyo ni sehemu ya kurudisha  ikhsani kwa jamii kutoka BSL.

Naye Mkaguzi Msaidizi  wa Polisi Kata ya Zinga A/ Insp. Mwajuma Msofe amesema kuwa Kata tisa boda boda na wananchi wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ikiwa lengo na lengo la  kupunguza matukio ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.

“Tunaushkuru uongozi wa BSL  kwa msaada mliotoa leo hii lakoni pia tunaomba  mtusaidie   pikipiki tano ambazo zitawasaidia  Polisi Kata katika kutekeleza  majukumu  yao ya kila siku kwa jamii” A/Insp. Msofe amesema.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Shaibu Ndemanga ameomba uongozi  wa BSL  kujenga vibanda na stendi za abiria ili waweze kutumia wakati wa kusubiri usafiri nakujikinga na hali za mvua na jua.

“Tunawashukuru sana BSL kwa msaada  huu kwa sababu  katika eneo hilo la Kata ya Zinga inatumiwa  na wanafunzi zaidi ya 1,000 ambao wanavuka kila siku kwenda na kurudi shuleni nawasisitiza wanafunzi, waalimu na raia wengine mzingatie kusimamia alama za usalama barabarani  ili  kuepuka vifo vya ajali za barabarani.” Amesema Ndemanga.

“Tunawaomba BSL mtujengee matuta na ikibidi daraja ili  raia wanafunzi wawe wanavuka kwa kupita juu huku magari yaendelee kupita chini kama ilivyojengwa  daraja la buguruni” amesema DC Ndemanga.

Sgt.Otilia Ponera ametoa  elimu kwa kata  tisa  ikiwamo boda boda na wananchi umuhimu wa   elimu ya usalama barabarani ikiwa lengo ni kupunguza matukio ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.

Baadhi ya wanafunzi  wakifuatilia maelekezo  kutoka kwa Sgt. Otilia Ponera maelekezo kwa vitendo  ya kuvuka barabara  kwenye alama za Pundamilia.

Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini  maelekezo  yaliyokuwa yakitolewa.

Afisa Utawala BSL  Ibrahim  Juma  Mohammed  amesema kuwa msaada  huo ni mwendelezo wa michango mbalimbali ambayo wamekua wakitoa huku akisisitiza kuwa kwa niaba ya uongozi amechukua maombi yaliyotolewa na kuahidi atayafikisha kwa uongozi  wa juu kwa utekelezaji.

Mkaguzi Msaidizi  wa Polisi Kata ya Zinga A/ Insp. Mwajuma Msofe akizungumza leo kwenye hafla hiyo .Tarehe 13 Januari 2025.

Related Posts