Che Malone Awaomba Radhi Mashabiki wa Simba – Global Publishers



Beki wa kimataifa, Che Malone kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Januari 14, 2025 amewaomba radhi mashabiki wa Simba na wadau wa soka kutokana na makosa aliyoyafanya likiwemo lililoigharimu Simba Januari 13, 2025 nchini Angola dhidi ya Bravos.

Kwenye mchezo huo, Simba ilipata sare ya 1-1 na kuipa nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Malone ameandika: “Ningependa kuomba radhi kwa familia nzima ya Simba kwa kuwagharimu sana katika siku mbili za michezo.

“Nachukua jukumu kamili kwa makosa yangu naahidi kufanya kazi kwa bidii ili niwe bora zaidi katika siku zijazo.
Pole sana. Asante Simba. Asante mashabiki kwa kunitia moyo kila wakati licha ya kukatisha tamaa kwangu.”











Related Posts