Mtambuka aamsha morali Songea United

KLABU ya Songea United ya mkoani Ruvuma imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa TMA ya jijini Arusha, Abiud Mtambuka kwa mkataba wa miezi sita, huku kocha wa kikosi hicho, Meja Mstaafu, Abdul Mingange akijivunia usajili wake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mingange alisema usajili wa mchezaji huyo utaongeza chachu ya ushindani ndani ya kikosi hicho katika kutimiza malengo ya kukipandisha Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, huku akiweka wazi anatambua vyema kipaji chake.

“Nilishawahi kufanya naye kazi nikiwa Mashujaa hivyo namtambua vizuri, ni mchezaji mzuri na naamini ataongeza morali na ushindani kwa washambuliaji wengine waliopo hapa, bado tunaendelea na mikakati ya kuboresha maeneo mbalimbali,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC, Mbeya City na Tanzania Prisons aliyejiunga na Songea United akitokea Stand United ya mkoani Shinyanga, aliongeza hawako nafasi mbaya sana ingawa wanapaswa kujipanga zaidi.

Related Posts