11 wafariki dunia ajalini Handeni, 13 wajeruhiwa

Handeni. Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo Kijiji cha Chang’ombe Kata ya Segera wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo imetokea baada ya basi aina ya Tata kupinduka na baadaye wananchi kujitokeza kusaidia ndipo lori linalodaiwa kufeli breki likawagonga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 13, 2024 na kusema miili imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Korogwe.

Amesema tayari baadhi ya miili imeshatambuliwa na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu, huku taratibu za kusafirisha miili kwa gharama za Serikali ikiendelea.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts