Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo amempongeza Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuaminiwa na Marais wa nchi nyingine katika nyanja ya Diplomasia.
DC Mpogolo, ametoa pongezi hizo leo kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC, wakati anazungumzia kuhusu ugeni wa Marais 54 kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika.
Kupitia mkutano wa Afrika wa Nishati Safi, Mkuu huyo wa Wilaya Ilala, ametumia nafasi hiyo kuzungumzia vivutio vya utalii vilivyopo Ilala vitakavyotembelewa, ni Soko la Samaki Fery, nyumba ya kupumzika ya zamani ya wakoloni ijulikanayo kama Ngome, Kumbi mbili za mikutano ya historia Karimjee na Anatoglo na vivutia vya sehemu za kupumzika.
Aidha, kufuatia mkutano huo unaotarajiwa kufanyika jijini dar es salaam kuanzia Januari 27-28 mwaka huu, DC Mpogolo, ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia vizuri mkutano huo kutangaza biashara zao kutokana na wageni wengi wanaokuja na taasisi za kimataifa.
Kuhusu suala la Usafi, ameeleza Ilala inaendelea na zoezi la usafi ili kuweka mandhari katika muonekano mzuri.