Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Methew amemtaka Mkandarasi STC CO LTD anaejenga chanzo cha maji katika Mto nyangao -Chiuwe kukamilisha kazi ndani ya miezi miwili.
Mhandisi Kundo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Wilayani Lindi kwenye mradi wa maji Nyangao- Mtama na mradi mkubwa wa vijiji 56 kwa kutumia chanzo hicho cha Mto Nyangao/Chiuwe Lindi kwenda Wilaya za Ruangwa na Nachingwea unaogharimu takribani Shilingi Bilioni 119.
Baada ya kukagua ametumia nafasi hiyo kuagiza hadi kufikia mwezi Machi,2025 wananchi wa mtama na Nyangao waanze kupata huduma ya maji kupitia mradi wao mpya ambao unatekelezwa na mkandarasi Halem Co Ltd.
Pia amemtaka Meneja wa RUWASA MKOA, Meneja wa Wilaya kukaa na mkandarasi Halem Co Ltd kwa ajili ya kufanya majadiliano kwa kazi inayoongezeka ili kazi hiyo ifanyike ndani ya mwezi mmoja
Kwa upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameidhinisha fedha nyingi za miradi ya maji Wilayani humo kiasi cha Shilingi 4.577Billion na mradi wa kutoka Lindi kwenda Ruangwa na Nachingwea kwa 119.1Billion, naye jukumu lake ni kusimamia na kuhakikisha miradi inajengwa kwa ubora ili idumu vizazi na vizazi na kuondoa kabisa adha ya maji kwa kumtua mama ndoo kichwani.