.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amefanya mazungumzo na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Justine Mhando, ambao wamefika Ofisini kwake Januari 13, 2025 wakiwa katika Ziara ya Kikazi ya Siku mbili ya Kukagua Mali za Shirikia hilo.
Katika Mazungumzo hayo Mwenyekiti Bwana Justine amehukakikishia Hajat Mwassa kuwa Shirika linaendelea na utoaji Elimu kwa Watanzania ili kuwa na uelewa wa Pamoja juu ya kuwa na Bima ya Maisha, Bima ya Elimu, Bima za Majengo pamoja na Vyombo vya Moto.
Mkuu wa Mkoa Hajat Fatma Mwassa amefurahishwa na ujio huo, na kuongeza kuwa kufika kwao katika Mkoa wa Kagera itaongeza chachu ya kuziunganisha pia Nyumba na Majengo ya Taasisi katika mpango wa Bima, tofauti na ilivyozoeleka kuwa Bima ni kwa ajili ya Magari tu na mambo mengine.
Mhe. Mwassa amesema ikiwa kila Mtu atafahamu vyema umuhimu wa kuwa na Bima, itasaidia sana kujikimu pale hata linapotokea tatizo na wakati huna akiba ya fedha kuweza kulitatua tatizo hilo.