Simba ya Fadlu yamkosha Azim Dewji

SIMBA imerudi nchini ikiwa na tiketi yake mkononi ya kucheza robo fainali ya sita kwenye mashindano ya Caf na kwenye msafara wa timu hiyo alikuwemo mfadhili wao wa zamani, Azim Dewji, ambaye ameshuka na maneno mazito juu ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Fadlu Davids.

Dewji katika mechi mbili za hivi karibuni ambazo Simba imeenda kucheza ugenini dhidi ya CS Sfaxien (Tunisia) na Bravos (Angola), amesafiri na kikosi hicho kilichokusanya pointi nne baada ya kushinda 1-0 na sare ya 1-1.

Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kuwasili kwa kikosi hicho kikitokea Angola, Dewji alisema amekoshwa na namna uongozi wa Bodi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Mohammed Dewji akisema hatua ya kwanza ya kukisuka kikosi hicho imefanyika kwa kiwango kikubwa.

Alisema, ameridhishwa na ubora wa wachezaji ambao wamesimama imara kwenye mechi za ugenini na hata za nyumbani huku akisema Simba ina nafasi ya kuongoza hata kundi lao.

“Kwanza niipongeze Bodi ya Wakurugenzi ya Simba chini ya Mohammed (Dewji), unajua mimi sijasafiri na Simba kwa takribani miaka 32, tangu niliposimama kuifadhili lakini hizi mechi mbili za ugenini nikasema acha niende nikaone timu inachezaje kwa macho yangu,” alisema Dewji na kuongeza.

“Nilikuwa Tunisia na sasa nimetoka Angola, kiukweli uongozi umefanya kazi ambayo Wanasimba walikuwa wakiililia, hiki kikosi ni bora naweza kusema hatua hii ya kwanza usajili umefanyika wa viwango.

“Unaona namna wachezaji wanacheza kwa ubora hasa hizi mechi za ugenini hata ile mechi ambayo tulipoteza ilikuwa ni makosa yetu na baada ya hapo vijana wakabadilika, kwa namna nilivyoiona Simba kule na tunarudi nyumbani tuna

Related Posts