Stein, Polisi wana balaa kikapu Dar

MSHIKEMSHIKE umeendelea kuonyeshwa na timu mbalimbali katika Ligi Daraja la Kwanza Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kuna vita kali ya kuwania kupanda Ligi Kuu ya Kikapu mkoani humo (BDL), huku Stein Warriors na Polisi zikiendelea kuonyesha umwamba.

Tukianza na Warriors, nguvu kubwa iliyotumiwa na PTW katika mchezo dhidi yake ilichangia timu hiyo kupoteza mchezo uliopigwa majuzi katika viwanja vya Bandari vilivyopo Kurasini jijini humo.

Katika mchezo huo Stein Warriors ilishinda kwa pointi 69-33 ambao PTW iliuanza kwa kuonyesha kukamia, lakini ikajikuta ikizimwa na mastaa wa wapinzania wao  walioonekana kucheza kwa utulivu.

Katika mchezo huo Stein Warriors iliongoza robo zote nne kwa pointi 19-12, 22-13, 12-19 na 22-2, huku   James Ngaboyed akifunga pointi 28 ambapo kati hizo alifunga ‘three points’ tisa na asisti tano.

Mchezaji huyo alifuatiwa na Abbas Omary aliyefunga pointi 18, huku Mohammed Jaffer wa PTW akifunga  tisa.

Related Posts