Dkt. Samia Afanya Uteuzi wa Viongozi Mbalimbali – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Mhandisi Ramadhani Masoud Lwamo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka Rais Samia pia amemteua Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili.

Vilevile Dkt. Samia amemteua Prof. Othman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili huku Dkt. Florens Martin Turuka akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kwa kipindi cha pili.

Aidha Rais Samia amemteua Prof. Valerian Cosmas Silayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kwa kipindi cha pili.











Related Posts