HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAKIMBIZA WAHUNI WOTE KWENYE MIRADI YA SERIKALI

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam imefuta mikataba yote ya ujenzi ambayo imekuwa ikisuasua katika utekelezaji na kuisababishia halmashauri hasara kubwa 

akizungumza wakati wa kusaini mkataba mpya na mkandarasi anayejenga shule ya sekindari kipunguni mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya ametaja kuwa wameamua kufanya uamuzi huo kufuata maelekezo yaliyotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa SGR.

Kwa upande wake mkuu wa  wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo amesema wao kama viongozi wanatekeleza agizo la Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati wa uzinduzi wa treni ya Mwendokasi(SGR) la kuwataka kukamilisha miradi inayowagusa wananchi moja kwa moja.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo leo Januari 15,2025 wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa umaliziaji wa jengo la ghorofa la shule ya sekondari Kipunguni.

“Tunaposema Serikali imedhamiria kutimiza yale inayoahidi,mfano ni ukamilishwaji wa jengo la shule hii ambao ni utekelezaji wa agizo la Rais alilotoa kwamba tuhakikishe miradi inakamilika”.Alisema Mkuu huyo wa Wilaya

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imedhamiria kukamilisha miradi yote iliyokwama kutokana na sababu mbalimbali na ukamilishaji huu wa miradi una lengo la kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo huduma za afya,elimu nk.

Related Posts