Tabora yabeba straika kutoka Tajikistan

DIRISHA dogo la usajili lilifungwa jana usiku, huku mapema juzi Tabora United ilikamilisha dili la kumsajili mshambuliaji mzawa Emmanuel Mwanengo aliyekuwa akiichezea Vakhsh Bokhtar iliyopo Tajikistan.

Klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tano katika Ligi Kuu Tajikistan (SSR Tajik League), Mwanengo aliitumikia kwa mwaka mmoja kabla ya dirisha la digo la usajili  kuamua kujiunga na Tabora United.

Rekodi za mshambuliaji huyo ambaye amekuwa hapati nafasi za kucheza sana zinaonyesha kuwa msimu huu amefunga mabao matatu katika ligi hiyo.

Usajili huo umefanyika baada ya dili la kumchukua Maabad Maulid anayekipiga Coastal Union kukwama kwa Tabora kurudishiwa pesa zao na KVZ inayommiliki mchezaji huyo, na mshambuliaji huyo mwili jumba kusalia kwa Wagosi.

Kutokana na dili la Maabad kukwama ndipo Tabora ikaamua kumgeukia Mwanengo ambaye alikuwa amemaliza mkataba na klabu aliyoitumikia ndani ya mwaka mmoja.

Awali, Mwanaspoti liliripoti kwamba kocha wa kikosi hicho, Anicet Kaizayidi alizungumza na mabosi wa klabu hiyo mapema na kuwapa mipango aliyonayo ikiwamo kupata nyota wapya kabla ya duru la pili kuanza.

“Kocha katika ripoti yake anataka mashine mpya sita mshambuliaji mmoja, viungo watatu, beki mmoja na kipa watakaoongeza nguvu katika druru la pili la ligi ili kujihakikishia kusalia katika nafasi nzuri zaidi ya hapa timu ilipo sasa,” ilielezwa taarifa ya awali ya klabu kuhusu mahitaji ya kocha Kaizayidi.

Kwa sasa Tabora inashika nafasi ya tano katika ligi, huku ikimaliza raundi ya kwanza kibabe kwa kuweka rekodi ya kuzifunga Yanga na Azam kwa mabao 3-1 na 2-1 mtawailia sambamba na kushinda mechi nne mfululizo za mwisho.

Related Posts