Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi wamewasili Mkoani Kagera Januari 15, 2025 kwa lengo la Kusikiliza na kupokea Kero na Changamoto zinazohusiana na masuala ya Kodi na Tozo mbalimbali.
Wajumbe hao wakiongozwa na Balozi Mwanaidi Maajar wamewasili Mkoani Kagera na Kukutana na Mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi. Fatma Mwassa, ambaye pamoja na mambo mengine ametoa ushauri na maoni yake juu ya masuala ya Kodi na njia za kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto.
Pamoja na hayo Wajumbe hao wamepata fursa ya kukutana na sehemu ya Viongozi wa Jumuiya za Wafanyabiashara pamoja na wawakilishi wa wafanyabiashara, ambao nao wamekuwa na mazungumzo nao katika cha awali kabla ya Kikao kingine ambacho watakutana na Wafanyabiashara na wadau wa Kodi.