Karakaba atabiriwa makubwa Namungo | Mwanaspoti

KOCHA wa Namungo, Juma Mgunda amemtabiria makubwa nyota wa Simba, Saleh Karabaka aliyetua katika timu hiyo kwa mkopo, huku akisisitiza amemvuta kiungo mshambuliaji huyo kutokaa na falsafa yake ya kuwaamini vijana wenye uwezo wa kucheza wakiwa na utulivu na akili kubwa uwanjani.

Karabaka aliyesajiliwa na Simba katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea JKU ya Zanzibar ametua Namungo kuungana na Mgunda aliyewahi kumnoa Msimbazi.

Akizungumzia usajili huo, kocha huyo wa zamani wa Simba na Coastal Union, alisema Karabaka aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Simba, licha ya kutopata nafasi alipotokea kwa upande wake anamuona  ni mchezaji mzuri na matunda yake yatakwenda kuonekana.

“Karabaka ukimwelekeza kitu cha kufanya wakati wa mechi anakitimiza kwa asilimia 100, kitu kilichomkwamisha ashindwe kuonyesha kiwango chake alijiunga Simba ikiwa na wachezaji wa kigeni wanaofanya vizuri katika nafasi yake, hivyo isingekuwa rahisi kwake kuwa chaguo namba moja,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Wachezaji vijana wanapaswa kujituma kwa bidii na kujifunza uvumilivu wa moyo pindi wanapokutana na changamoto ya kupata namba, ukifika muda wao naamini watacheza tu, mfano mzuri ni kina Edwin Balua, Ladack Chasambi ambaye kwa sasa anapewa nafasi ya kucheza na anaonyesha uwezo wake.”

Mgunda pia alimzungumzia Jean Baleke aliyekuwa Yanga kabla ya kuelezwa ametemwa katika dirisha dogo, kwamba amekuwa akizungumza naye mara kadhaa, ili kuwa mvumilivu kutokana na umri alionao kwani akitulia huwa ni mchezaji anayejua kufunga mabao.

“Huwa nazungumza na Baleke mara kwa mara kumtaka awe mvumilivu katika kazi yake,” alisema Mgunda.

Related Posts