NIC, BENKI YA EQUITY WASAINI MIKATABA KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Kaimu Mkeyenge Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya kifedha. Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam leo Januari 16, 2025.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

BENKI ya Equity imesaini Makubaliano na  Shirika la Bima la Taifa  (NIC)

kwa lengo la kufanya kazi kwa pamoja kwa na kusukuma mbele uchumi kupitia sekta ya fedha. 

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Januari 16, 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kaimu Mkeyenge amesema wameona ni muhimu wa kuziwezesha benki za biashara kwa kuzipa mitaji kutokana na ada ambazo NIC wanakusanya kutoka kwa wateja mbalimbali. 

“Hii ni moja ya njia ya uwekezaji kwa kuwekeza katika benki za biashara zilizopo hapa nchini ili ziweze na uwezo wa kukopesha kila mtu anajua ukwasi ni mhimu sana katika benki za biashara ili wananchi, wawekezaji wanaokuja nchini waweze kukopesheka mwisho wa siku tuweze kufanya shughuli za kiuchumi bila kutetereka.” Amesema Mkeyenge

Amesema makubaliano hayo yataiwezesha Equity benki kuongeza mtaji wao mtaji lakini NIC kupata maerejesho ya ambayo yatatokana na uwekezaji wa fedha hizo.

Amesema katika hilo NIC watatumika kama kampuni ya bima ambayo itakata bima ya mikopo ambayo itakuwa ikikopesha.

Lakini pia amesema watashirikiana katika kutoa huduma bima kwenye sekta ya kilimo.

“Tuwahakikishie ambao watakuwa wanapata huduma za mikopo au huduma mbalimbali kupitia Equity benki watakuwa salama kwa sababu NIC itaingia makubalino ya kufanya kazi pamoja na kukata bima katika sekta ya Kilimo.” Amesema

Mashirikiano hayo yataleta faida baina ya taasisi hizi mbili za fedha vile vile kutoa mchango katika uchumi wa nchi na maendeleo ya watanzania lakini pia kuisaidia serikali kuitimiza azma yake ya kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga amesema  benki inapofanya kazi ya kutoa huduma za bima haiwezi kufanya kazi peke yake bali ni lazima ishirikiane na taasisi za bima ambazo zenyewe zina wigo mpana na uwezo mkubwa katika kutoa huduma na ushauri.

“Sasa kwa kutambua  ukubwa huo na uwezo huo wa shirika la bima la Taifa (NIC) sisi Equity Benki tukasema tuwe na mahusiano  ya kimkakati  ambayo taasisi zetu mbili  tunaweza tukafanya kazi pamoja  na katika  kuanzisha mahusiano hayo ya kimkakati  tumeangalia huduma ambazo sisi tunazitoa ndani na tumezipa kipaumbele  zina uhitaji mkubwa  wa wateja na zinauhizaji mkubwa wa soko,”alisema Maganga

Ameongeza kuwa Katika kuangalia hilo benki hiyo imetoa kipaumbele katika sekta ya kilimo lakini katika madaraja ya wateja  tumetoa kipaumbele  kwa wafanyabiashara  wadogo na wakati kidijitali.

Amesema kwa  mwaka 2024 ni asilimia 60 ya wateja wamepata mkopo kwa njia hiyo na Sh. bilioni 3000 zilitolewa kupitia mitandao ya kidijitali waliyonayo. 

Maganga amesema watu hao wanahitaji kulinda na majanga yanayoweza kutokea muda wowote ndio maana tukavutiwa kufanya kazi na Shirika hili la bima kwani ni wateja zaidi ya elfu 20 wanatumia huduma hizo.

Amesema uhitaji wa bima kwa jamii bado ni mkubwa hivyo elimu iendelee kutolewa ili watu waweze kukata bima mbalimbali zinazotolewa ilikuepuka gharama zisizoza lazima kwani ukiwa na bima kila kitu kitalipwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Kaimu Mkeyenge Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga wakionesha mikataba mara baada ya kuisaini jijini Dar es Salaam leo Januari 16, 2025.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Kaimu Mkeyenge Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga wakibadilishana mikataba.

Related Posts