Na Mwandishi Wetu,Geita
MPANGO wa kunusu kaya maskini nchini (TASAF) umetumia zaidi ya Shilingi bilioni 59 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na fedha kwa ajili ya walengwa wa mpango huo kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Januari 2025 Mkoani Geita.
Akizungumza wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya uongozi Tasaf makao makuu waliofika mkoani Geita kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa kwa fedha za Tasaf,Katibu Tawala Mkoa wa Geita Mohamed Gombati amesema uwepo wa mpango umewezesha watoto wa walengwa wanaosoma shule za msingi na sekondari kumudu kupata mahitaji ya shule na kuendelea na masomo.
Amesema mpango huo umesaidia kuongeza mahudhurio ya kliniki kwa watoto chini ya miaka mitano na wazazi kupata mafunzo na malezi ya watoto,huku baadhi ya walengwa wakifanikiwa kuanzisha biashara ndogondogo kwa ajili ya kupata kipato na kuimarisha uchumi wa kaya.
“Walengwa wengi wamemudu kupata mahitaji ya msingi katika kaya na kuweza kumudu kupata milo miwili tofauti na awalai hali zao zilivyokuwa kabla ya mpango”amesema
Katika ziara hiyo ya siku moja Wajumbe hao wa kamati ya Uongozi Tasaf makao makuu wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Nyabilezi kilichopo Wilayani Chato kilichojengewa kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.4 ambazo ni fedha za Tasaf.
Akizungumza katika kituo hicho Mganga mfawidhi wa kituo Sylivester Bundalah amesema kupitiaTasaf miradi kumi ya miundombinu imetekelezwa kwenye kituo hicho.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi waa jengo la wagonjwa wa nje,Jengo la maabara ,jengo la upasuaji na lile la wazazi,nyumba ya kuhifadhia maiti,kichomea taka ngumu,nyumba za watumishi,jengo la kufulia,ujenzi wa vyoo,uzio pamoja na njia ya kupita wagonjw ana watumishi.
Amesema kukamilika kwa kituo hicho kumewaondolea wananchi zaiid ya 12,000 adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya kwenye hospitali ya Wilaya iliyoko umali w akm 18.
Amesema pamoja na kuwaondolea wananchi adha ya kutembea umbali mrefu bado wanalazimika kufuata huduma mbali pale wanapohitaji matibabu makubw akutokana na vifaa vilivyopo kituoni kushindwa kufanya kazi kutokana na kituo kukosa umeme wa njia tatu.
Wakizungumza mara baada ya kutembelea kituo hicho wajumbe wa kamati ya uongozi Dk Ruth Lugwisha na Dk Naftali Ng’ondi w ameutaka uongozi wa halmashauri kwa kushirikiana na uongozi w a kituo kuona namna ya kufunga umeme mkubwa kwenye kituo hicho ili vifaa hivyo viweze kutumika.
“Vitu vya umeme visipotumika vinaharibika Halmashauri angalieni uwezekano wa kupata fedha hata kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya kufunga umeme mkubwa kwenye kituo hiki ili lengo la Serikali la kutoa vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa liwe na tija”amesema N’gondi
“Hivi ni vitu vya gaharama halmashauri na uongozi wa hospitali kaeni chini muone njia ya kuleta umeme mkubwa hapa ,mfano kuna Wafanyabiashara ,kuna watu wakubwa hapa kuna viwanda washirikisheni naimani hawatakataa ili vifaa hivi viweze kutoa huduma”amesema Dk Lugwisha.
Katika hatua nyingine Wajumbe hao wa kamati ya uongozi ya Tasaf wameshauri walengwa wa Tasaf waelimishwe ili watambue kuwa Umaskini sio sifa nzuri hivyo wanapaswa kutumia kidogo wanachopokea kwa malengo ili baada ya muda watoke kwenye lindi la umaskini na kujitegemea.