Na Mwandishi wetu Dodoma
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limependekeza likizo ya dharura ambayo haitakua na malipo kwa mfanyakazi mwenye uhitaji iwe angalau miaka 5 ili kukidhi mahitaji ambayo huenda yakawa ni ya kiuongozi ama kimasomo badala ya siku 30 iliyopendekezwa na muswada.
hayo yamekuja baada ya Mapendekezo kuhusu Maoni ya Marekebisho ya Sheria za Kazi kwa Mwaka 2024 yaliyowasilishwa mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya ustawi na maendeleo ya jamii yaliyotolewa mnamo tarehe 15 Januari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma. ambapo Tucta imetolea mapendekezo ambayo wanaamini yatakubaliwa na kufanyiwa kazi huku sehemu kubwa ya mapendekezo hayo yakipingana na maoni yaliyotolewa na Kamati hiyo ya kudumu ya Kudumu ya Bunge.
Akitoa Taarifa kwa Wanahabari leo tarehe 16 Januari, 2025 Jijini Dodoma. Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Peter Nyamhokya amesema Shirikiaho hilo linashauri pia nafuu ya mtu anayesitishiwa ajira kwa kutokufuata taratibu au kutokuwepo na sababu zenye mashiko basi alipwe fidia au nafuu ya mishahara kulingana na sheria iliyopo sasa tofauti na mapendekezo ya muswada ambayo yameweka ukomo wa mishahara isiyozidi miezi 12.
“Mapendekezo ya muswada uliopo sasa yatasababisha uwepo wa fidia zisizo na uhalisia na pia kuwapa mamlaka waajiri kusitisha ajira za wafanyakazi pasipo kufuata utaratibu.”
“Lakini pia itaondoa maana ya uwepo wa kanuni za utendaji bora tangazo la serikali namba 42 la mwaka 2007 (code of good practice). TUCTA inashauri vyombo vyetu vya utatuzi wa migogoro ya kikazi nchini vimekuwa vikifanya kazi yake kwa umahiri mkubwa kwa kutoa fidia zinazostahiki kwa kuzingatia sheria iliyopo sasa.” ameeleza Rais huyo.
Tucta inapendekeza pia mfanyakazi anayejiriwa kwa misingi ya kupata mafunzod (trainee) afanye mafunzo hayo kwa kipindi cha miezi isiyozidi 12 tu kisha aajiriwe kama mfanyakazi kamili badala ya miezi 24 iliyopendekezwa na muswada.