BARAZA La Sanaa la Taifa (BASATA) Limesema Milango ipo wazi Kwa Wadau wenye Mawazo ya kibunifu kwa lengo la kukuza tasnia nchini Tanzania na Kuongeza vipato vyao.
Akizungumza jana January 15,2025 Jijini Dar es Salaam na Wanahabari Wachekeshaji na Wadau wa Tasnia hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. kedmon Mapana amesema kimekuwa kilio cha muda mrefu kwa Wasanii wa ucheshi Kuhitaji Tuzo hizo ili waweze Kutambulika na Kuendelea Kukuwa Kwa Kazi zao kutokana na Kuwepo ushindani wa Kazi zao Kila siku.
Hata hivyo Mapana ameeleza Kwakina Kuwa Muasisi na Mbeba Maono wa Tuzo hizo Omary Nyembo maarufu Kama “Ommy dimpoz” ameweka mikakati mizuri kuhakikisha tuzo hizo mpya zinatambua mchango wa Wasanii hao na Kazi zao Kwa kuweka muendelezo mzuri mara baada ya kushinda tuzo hizo.
Pia Mapana ameweka Wazi Kuwa Baraza lake (BASATA) Linafungua Milango wazi Kwa Wadau wenye Mawazo ya Kibunifu Kwa ajili ya Kukuza Maendeleo ya Sanaa ya Tanzania.
“Tumempokea Dimpoz na wazo lake la kibunifu la kuanzisha tuzo hizo na tukampa mikakati apite wapi kuhakikisha wazo linaenda kuwa kiuhalisia na uzuri tuzo zimekuja msukumo mkubwa wa Kuwepo kwa Wadau ambao watahakikisha Tuzo zinafanyika kwa asilimia zote .”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu Dkt.Gervas Chuma amesema Kuwepo kwa Tuzo hizo itachangia Kukuza vipaji vingi vipya katika tasnia ya ucheshi nchini.
Hata hivyo amesema tuzo hizo zitawaniwa 21 ndani yake kutakuwa na tuzo ya Mchekeshaji bora wa mwaka upande wakike na upande wakiume, video bora ya mwaka ya ucheshi ,chawa bora mwaka pamoja na zingine nyingi.
Nae Muasisi wa tuzo hizo za Ucheshi Omary Nyembo “Ommy Dimpoz ” amesema tuzo hizo zimedhaminiwa na Wadau mbalimbali akiwemo Silent Ocean pamoja ambapo zimetengwa pesa kwa ajili ya Watakaoibuka Washindi .
“Mchekeshaji bora wa Mwaka ataondoka na milioni 30,Mchekeshaji bora wakike ataondoka na milioni 20,Mchekeshaji bora wakiume ataondoka na milioni 20 huku Kila mshindi wa kipengele ataondoka na milioni 5 “.