MUFTI MKUU TANZANIA AWASILI DODOMA KUUFUATA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI

 Wageni waalikwa wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamewasili salama jijini Dodoma tayari kushiriki kikao cha ufunguzi kinachotarajiwa kufanyika kesho, tarehe 18 Januari.

Akizungumza mara baada ya kuwasili, mmoja wa wageni hao, Muft Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir, alieleza shukrani zake kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwafanikisha safari yao kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

“Tumefika salama kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Ni heshima kubwa kwetu kuwa sehemu ya tukio hili muhimu la kihistoria. Tumealikwa kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo pamoja na kufunga,” alisema Sheikh Abubakar Zubeir

Aliambatana na ujumbe mzito wa viongozi wa dini wakiwemo Sheikh Mustafa Rajab, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Khatibu Kazungu wa mkoa huo, Sheikh Yusufu Tonge, mjumbe wa Halmashauri Kuu, na Sheikh Omar, pia mjumbe wa Halmashauri Kuu. Viongozi wengine walioungana nao ni Sheikh Haruna Kichwabuta, Sheikh wa Mkoa wa Kagera.

Sheikh Zubeir alisisitiza kuwa mwaliko huo ni utukufu mkubwa na heshima kwa viongozi wa dini waliowakilishwa. “Ni jambo kubwa kuwa hapa kama wageni waalikwa kushuhudia na kushiriki hatua muhimu katika historia ya CCM,” aliongeza.

Related Posts