Shule ya Msingi Holy Peak ya Arusha mwamba Kitaaluma

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Shule ya Msingi ya Msingi ya Holy Peak ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha imepania kutoa elimu bora kwa Vijana wa kitanzania ili kukuza vipaji vyao.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Mchepuo wa Kiingereza Hans Mara anasema kuwa kufanikisha lengo hilo inatilia mkazo sera mpya ya elimu inayotilia mkazo elimu ya vitendo na kukuza vipaji.

“Tunaunga mkono sera hiyo na ndiyo maana tunaongoza katika matokeo na miongoni mwa shule za kanda yetu ya Kaskazini,” anasema Mwalimu Hans

Kwa Mfano anasema kuwa mwaka 2024, shule imeshika nafasi ya juu zaidi kwani kiwilaya imeendelea kuwa ya kwanza kimkoa ya kwanza (1) na ndani ya kanda ya kaskazini ihusishayo mikoa kama Arusha, Manyara, Kilimanjaro pamoja na tanga bado shule imejitanabaisha kwa kuwa bingwa kitaaluma kwa kushika nafasi ya kwanza.

Anasema Kitaifa ni miongoni mwa shule kumi (10) bora imepata daraja “A–Bora” kwa wastani na 291.7500/300.

Mwaka 2022, matokeo ya darasa la saba yaliiwezesha shule kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na nafasi ya tano kimkoa kwa kupata daraja “A – Bora” kwa wastani wa alama 265.9545/300.

Mwalimu Hans aasema mwaka 2023 matokeo ya darasa la saba, shule ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na ya nne Kimkoa, ufaulu ulikuwa juu na kupata daraja “A- Bora” kwa wastani wa alama 264.7308/300.

Anasema sababu ya wao kuongoza ni pamoja na kuwa na waalimu wabobezi katika taaluma ya ualimu na malezi bora kwa watoto pia ina kitengo maalumu cha ushauri nasaha kwa wanafunzi na watumishi.

Shule ina mazingira safi, tulivu na salama kwa kujifunzia na kufundishia, Shule ina maktaba ya kisasa yenye vitabu vya kutosha,Shule inafundisha fani mbalimbali zinazo ibua vipaji vya watoto ikiwemo michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, pete na mpira wa kikapu.

Shule ina magari ya kutosha kwa wafunzi wa kutwa,Shule inawalea wanafunzi katika maadili bora kwani inavipindi maalumu vya dini kulingana na dini ya mwanafunzi husika.

Mahali shule ilipo Kama utatokea Moshi / Arusha mjini utashuka kituo cha Maji ya chai, upande wa mashariki utaona kibao cha shule kilichopo mkabala na barabara ya kuelekea Doli ambapo ni kilometa 1 kufika shuleni.

0787858740 – Mkuu wa shule

0767265593 – Mkurugenzi wa shule 

Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Holy Peak ya Wilayani Meru Mkoa wa Arusha
katika matukio mbalimbali .

Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Holy Peak ya Wilayani Meru Mkoa wa Arusha
katika matukio mbalimbali .

 

Related Posts