Tamu, chungu kuahirishwa Chan 2024

Uamuzi wa kusogezwa mbele fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) 2024 hadi Agosti mwaka huu unaweza kuja na faida chanya na hasi hasa kwa Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi tatu wenyeji wa mashindano hayo.

Jumanne, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) lilitangaza kuwa fainali hizo ambazo zilipangwa kufanyika kuanzia Februari Mosi hadi Februari 28 mwaka huu zitachezwa Agosti kutiokana na kutokamilika kwa maandalizi yake kwa nchi wenyeji ambazo ni Kenya, Uganda na Tanzania.

Maoni mbalimbali ya wadau wa mpira wa miguu, yamefafanua kuwa uamuzi huo unaweza kuwa na neema kwa upande mmoja lakini ukageuka shubiri upande mwingine.

Kupatikana kwa muda mrefu wa maandalizi ya mashindano hayo inaonekana kuwa faida kubwa ya kuahirishwa kwa Chan 2024, jambo ambalo litafanya nchi wenyeji kama Tanzania kukamilisha sehemu ndogo iliyobakia ya maandalizi na kuiboresha ili kuzifanya fainali hizo kuwa bora zaidi ya hata ambavyo zingefanyika Februari.

“Tunayo miezi sita zaidi ya kujiandaa na Chan na kusema kweli tulikuwa tumekaribia kabisa kuwa tayari kwa asilimia 100. Lakini miezi sita hii pamoja na mchakamchaka tuliokimbia katika miezi ya hivi karibuni kujiandaa na Chan, imetupa ufahamu mkubwa wa namna mambo haya yanavyotakiwa kuwa, niwahakikishie miezi sita hii tutaitumia vizuri na tutakuwa na Chan bora zaidi kuliko ambayo ingefanyika kwa mwezi unaofuata,” alisema naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’.

Kurejea mapema kwa Ligi Kuu Tanzania bara ni faida nyingine ambayo kusogezwa mbele kwa Chan 2024 kumeileta kwa Tanzania tofauti na iwapo ratiba ya awali ingebaki kama ilivyo.

Iwapo mashindano ya Chan yangefanyika Februari mwaka huu, Ligi Kuu bara ingerejea mwezi Machi jambo ambalo lingesababisha viporo kwa timu, ratiba inayozibana klabu mara baada ya Chan kumalizika na pia kulikuwa na uwezekano mkubwa wa ligi kuchelewa kumalizika.

Na kuthibitisha hilo, muda mfupi baada ya Chan kusogezwa mbele, bodi ya Ligi Kuu Tanznaia (TPLB) jana ilitangaza kurejea kwa ligi mwanzoni mwa Februari.

“Bodi ya Ligi Ku Tanzania (TPLB) inatangaza mabadiliko ya tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo hapo awali ilipangwa kuendelea Machi 1, 2025 baada ya kutamatika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi na fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Michezo ya Ligi Kuu ya NBC sasa itarejea katika juma la kwanza la Februari, 2025 kwa michezo ya ‘viporo’ kabla ya kuendelea na michezo ya munguko wa 17. Tarehe rasmi pamoja na ratiba iliyofanyiwa maboresho, zitatangazwa hivi karibuni,” ilifafanua taarifa ya TPLB.

Hata hivyo kuna athari kadhaa hasi ambazo zinaweza kuletwa kutokana na kuahirishwa kwa fainali hizo, mojawapo ikiwa ni kuingiliana na ratiba za mashindano mengine.

Mchambuzi wa soka na kiungo wa zamani wa AFC Arusha, Ibrahim Masoud  alisema kuwa athari ya kuingiliana na kalenda nyingine ni kubwa.

“Wasiwasi wangu tarehe za kufanyika Chan zinaweza zisiwe rafiki na kuendana na ratiba ya kidunia. Agosti ni kipindi cha maandalizi ya msimu mpya na ni ngumu hata kwa mawakala wa soka kuja kutazama mashindano ili kusaka wachezaji lakini pia kwa Tanzania hicho ni kipindi cha kuelekea tukio kubwa la Uchaguzi Mkuu wa nchi,” alisema Masoud.

Makamu mwenyekiti wa Singida Black Stars, Omary Kaya alisema kuwa athari nyingine inaweza kuwa ni kuharibu taswira ya nchi.

“Kuleta taswira mbaya kwa kuonyesha mapungufu makubwa kwenye uandaaji wa mashindano makubwa wa haya mashindano.Hili liwe fundisho na ukumbusho kwa maandalizi ya Afcon maana nchi ni hizi hizi na tumeona mapungufu hivyo yafanyiwe kazi kuondoa hii aibu,” alisema Kaya.

Biteko aanika fursa Chan, Afcon

Katika hatua nyingine, jana naibu waziri mkuu na waziri wa nishati, Dk Doto Biteko jana alitoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) 2024 na Afcon 2027 kwa vile mashindano hayo mawili yana faida kubwa kwa nchi na mtu mmojammoja.

Akizungumza katika kongamano la wadau wa michezo kuelekea Chan 2025 na Afcon 2027 jijini Dar es Salaam, Biteko alisema Tanzania inayapa uzito mkubwa mashindano hayo kwa vile yana faida chanya hasa za nje ya uwanja.

“Nchi yetu imepata heshima kubwa kimataifa na hii haiji kwa bahati mbaya imesababishwa na ukuaji wa demokrasia iliyojengwa na Rais Samia kwenye mataifa mbalimbali duniani.

“Fursa za mashindano haya zitakuza uchumi wa nchi yetu na kufanya vikundi vya watu au kampuni mbalimbali kufanya biashara na kukuza uchumi wao na hatimaye kuondoa umaskini miongoni mwetu,” alisema Biteko.

Biteko alisema kuwa, mashindano yatawakutanisha wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali na kuna wajibu wa kufanya maandalizi kwa ufanisi mkubwa ili kunufaika na mashindano kupitia fursa mbalimbali za usafirishaji, malazi na burudani.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwijuma amesema lengo la kongamano ni kupokea maoni ya wadau mbalimbali na kuchanganua fursa zitakazokuja pamoja kuelekea mashindano ya Chan 2025 na Afcon 2027 ambazo watanzania watanufaika nazo.

Related Posts