TUME YA RAIS YA MABORESHO YA KODI YAKUTANA NA WADAU WA KODI MKOA WA SHINYANGA KUKUSANYA MAONI

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, CPA Leonard Mususa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi imefanya mkutano na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu uzoefu, changamoto na mapendekezo ya namna ya kuboresha mifumo ya kodi nchini.

Mkutano huo umefanyika leo, Ijumaa, Januari 17, 2025, katika ukumbi wa Lyakale Mjini Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi.

Akifungua mkutano huo, Wakili Mtatiro amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa wadau katika michakato ya kuboresha mifumo ya kodi, akisema kuwa michango na maoni yao ni muhimu na yatatumika kama sehemu ya mikakati ya kuleta mageuzi ya kimsingi katika sekta ya kodi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Mwanamapinduzi wa kweli, anayehamasisha na kusikiliza maoni ya wananchi. Anachukua hatua za haraka ili kuhakikisha kuwa maoni ya wananchi yanatekelezwa kwa manufaa ya wengi. Tume hii ya Rais haiachi jambo lolote nyuma, inazingatia taaluma na weledi wa hali ya juu katika kufanya tathmini ya mifumo ya kodi. Hivyo, michango yenu inachukuliwa kama maoni muhimu kwa kuboresha mifumo ya kodi na itafanyiwa kazi,” amesema Wakili Mtatiro.

Wakili Mtatiro amesema changamoto za kodi ni changamoto za kitaifa na kuahidi kwamba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kujitahidi kuboresha mifumo ili kuhakikisha kuwa masuala ya kodi yanakuwa endelevu na yanahusisha pande zote kwa faida ya nchi nzima.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, CPA Leonard Mususa, ameeleza kuwa tume hiyo inaendelea kufanya tathmini ya kina kuhusu mifumo ya kodi, mapato na tozo mbalimbali zinazohusiana sekta ya kodi.Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, CPA Leonard Mususa

Amesema kazi hii inaimarisha juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa mfumo wa kodi unakuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, na kwamba tume inashirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kodi zinakusanywa kwa njia bora na yenye haki, huku ikifanya mabadiliko ili kuondoa kero na malalamiko ambayo yamekuwa yakichochea malumbano.

“Tume ya Rais inatekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa ili kuondoa kero za kodi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Tume hii imelenga kuvutia mitaji ya ndani na nje ya nchi na kwa upande mwingine, tunafanya tathmini ya kina ili kuona ni hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa ili kuboresha mifumo ya kodi nchini,” ameeleza CPA Mususa.

Mkutano huo umetoa fursa kwa wadau muhimu wa masuala ya kodi wa Mkoa wa Shinyanga kutoa maoni yao kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika masuala ya kodi.

Wadau hao pia wamependekeza njia mbalimbali za kutatua changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kupunguza urasimu katika ukusanyaji wa kodi, kuboresha mawasiliano kati ya serikali na wafanyabiashara na kuongeza ufanisi katika utendaji wa mifumo ya kodi.

Mkutano huu ni sehemu ya juhudi za Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kukusanya maoni ya wadau kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwezesha mabadiliko ya mifumo ya kodi kwa namna itakayowafaidisha wananchi na nchi kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza leo Ijumaa Januari 17,2025 kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu uzoefu, changamoto na mapendekezo ya namna ya kuboresha mifumo ya kodi nchini. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, CPA Leonard Mususa akizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, CPA Leonard Mususa akizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga David Lyamoga kizungumza kwenye mkutano wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga
Wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kukusanya maoni kuhusu uzoefu, changamoto na mapendekezo ya namna ya kuboresha mifumo ya kodi nchini.

Wadau wa masuala ya kodi Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi ili kukusanya maoni kuhusu uzoefu, changamoto na mapendekezo ya namna ya kuboresha mifumo ya kodi nchini.

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Related Posts