CCM yatangaza muundo mpya wa wajumbe, uteuzi wa wagombea

Dodoma/Dar es Salaam. Hatua ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya mabadiliko ya Katiba yao huenda ikazua maumivu kwa wagombea ubunge na udiwani.

Mabadiliko hayo yamefanywa na Mkutano Mkuu wa chama hicho, jijini Dodoma leo Januari 19, 2025, mbele ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Akisoma mabadiliko hayo, Katibu wa NEC, Oganaizesheni Taifa, Issa Gavu, amesema mabadiliko hayo yamegusa pia nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu. Gavu amesema mabadiliko hayo yanahusu kuongezeka pia kwa idadi ya wajumbe watakaopiga kura za maoni kwa wagombea wa udiwani na ubunge.

Gavu amesema mabadiliko mengine yanayohusu Ibara ya 47(1), 60(1) na 73(1) ya Katiba hiyo. Kamati Kuu itakuwa na wajumbe 10 watakaochaguliwa kutoka Bara na Zanzibar, watano kila upande.

Kati ya wajumbe hao wa kuchaguliwa, amesema mabadiliko hayo yanatoa sharti la ulazima wa kati ya wajumbe hao wanne wanapaswa kuwa wanawake, yaani wawili kutoka Bara na wawili Zanzibar. Marekebisho hayo yatahusisha Ibara ya 103 (12F) na 104(1s) ya Katiba ya CCM.

Gavu amesema kwa sasa ibara hizo zinawataka wajumbe watakaopiga kura za maoni kwa wagombea hao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa kata au wadi, wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya.

Katika mabadiliko ya sasa, amesema wajumbe watakapiga kura za maoni kwa wagombea wa ubunge na udiwani ni wajumbe wote wa Kamati ya Siasa ya kila tawi, kata za jimbo au wilaya husika.

Pia, amesema wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya kila shina katika kata au jimbo au wilaya na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji katika kila tawi na kata ya eneo husika.

Kwa upande wa mjumbe wa Shina la CCM, Gavu amesema sasa atakuwa kiongozi wa nyumba zisizozidi 20 zenye wanachama wasiopungua 50 na wasiozidi 80 kwa mijini, huku wanachama 30 na wasiozidi 80 kwa vijijini kutoka 10 za awali.

Mabadiliko hayo yanaondoa utaratibu uliokuwepo kuwa shina la CCM linaundwa na nyumba 10 bila kuweka wazi idadi ya wanachama wanaopaswa kuwepo katika eneo hilo.

Marekebisho mengine, amesema yanahusu Ibara ya 9 ya chama hicho, ili kuondoa sharti la kujaza fomu kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mwanachama wa CCM, hivyo kuanzia sasa atatoa taarifa kwa Katibu wa chama hicho wa tawi husika.

“Mtu anayetaka kuwa mwanachama wa CCM, atawasilisha maombi yake kwa Katibu wa Tawi analoishi na yale masharti ya kujaza fomu yanakuwa yameondoka,” amesema.

Mabadiliko hayo, kwa mujibu wa Gavu, yamegusa pia nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu. Kamati Kuu pamoja na wengine, itakuwa na wajumbe 10 watakaochaguliwa kutoka Bara na Zanzibar, watano kila upande. Kati ya wajumbe hao wa kuchaguliwa, amesema mabadiliko hayo yanatoa sharti la ulazima wa kati ya wajumbe hao wanne wanapaswa kuwa wanawake, yaani wawili kutoka Bara na wawili Zanzibar. Marekebisho hayo yatahusisha Ibara ya 103 (12F) na 104(1s) ya Katiba ya CCM.

Kuongezeka kwa idadi ya wajumbe watakaopiga kura za maoni kwa wagombea wa udiwani na ubunge, amesema ni mabadiliko mengine yanayohusu Ibara ya 47(1), 60(1) na 73(1) ya Katiba hiyo. Gavu amesema kwa sasa ibara hizo zinawataka wajumbe watakaopiga kura za maoni kwa wagombea hao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa kata au wadi, wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya. Katika mabadiliko ya sasa, amesema wajumbe watakapiga kura za maoni kwa wagombea wa ubunge na udiwani ni wajumbe wote wa Kamati ya Siasa ya kila tawi, kata za jimbo au wilaya husika.

Pia, amesema wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya kila shina katika kata au jimbo au wilaya na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji katika kila tawi na kata ya eneo husika.

Mabadiliko mengine, amesema ni ya Ibara ya 91(6, c), ili kutoa jukumu kwa kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa kuchuja majina ya wagombea wa udiwani na Kamati Kuu kuchuja wagombea wa ubunge na Baraza la Wawakilishi.

Baada ya taarifa ya mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan, amesema muundo wa shina umelenga kuwapa wajumbe wa mashina idadi ya watu wa kuwaongoza na siyo nyumba kama ilivyokuwa. Kuhusu kuondolewa utaratibu wa mtu kulazimika kujaza fomu ili awe mwanachama wa CCM, Samia amesema kwa sababu kwa sasa kuna njia lukuki za kiteknolojia zinazomwezesha mtu kutoa taarifa.

Nyongeza ya idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu, Mwenyekiti huyo amesema ni mabadiliko yanayolenga kuongeza wajumbe wanaowakilisha sauti za wanachama, badala ya wale wanaoingia kwa vyeo vyao. Kwa upande wa nyongeza ya wajumbe watakaopiga kura za maoni kwa wagombea wa ubunge na udiwani, amesema wanalenga kuongeza idadi ya wanachama watakaopendekeza wagombea wanaowahitaji.

“Wale waliozoea kucheza na wajumbe wajipange, watakuwa wengi kidogo,” amesema Samia.

Related Posts