NYOTA wa kimataifa wa soka la wanawake, Clara Luvanga amezidi kutakata baada ya wikiendi iliyopita kutupia mabao mawili yaliyoisaidia timu ya Al Nassr kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Qadsiah, huku mtandao wa klabu hiyo ukimpaisha kwa kusema ‘hakuna wa kumzuia kutupia’.
Al Nassr ilipata ushindi huo ikiwa uwanja wa nyumbani wa Al Nassr na kuifanya izidi kujikita kileleni ikifikisha pointi 33 kutokana na mechi 11 ilizocheza na kushinda zote.
“Hakuna wa kumzuia Clara wetu Mashaallah, sababu za kupendeza zaidi za furaha nikuelezeje?” ni maandiko yanayochapishwa kwenye ukurasa wa Al Nassr kumfagilia Clara Luvanga.
Kila anapofanya vizuri nyota huyo, Nassr wamekuwa wakiposti picha na baadhi ya video wakiambatanisha na ujumbe mbalimbali.
Clara sasa amefikisha mabao saba na assisti nne kupitia mechi hizo 11.