Na Khadija Kalili Michuzi Tv
Timu za soka Kata ya Kisarawe na Kurui jana zimetoka sare ya goli moja moja ikiwa ni katika hatua ya kuwania kucheza mechi ya fainali ya michuano ya Jafo Cup itakayochezwa Februari 2 ,2025.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ambayo wachezaji wa timu zote wameonesha uwezo wa hali ya juu kwa kusakakata kabubu yenye viwango kwenye mechi iliyochezwa katika Uwanja Mzenga Wilayani Kisarawe Mkaoni Pwani jana jioni tarehe 18 Januari 2025.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mechi hiyo Kapteni wa timu ya Kisarawe Jonathan Mabuya amesema kuwa anamshukuru mungu mchezo mzuri na kusisitiza kuwa matokeoni matatu kushindwa kutoa sare na kutolewa .
“Mchezo wa leo umeshapita tunawaahidi mashabiki wetu wa Kisarawe kuwa kwenye mechi ya marudiano tutashinda” amesema Mabuya.
Kapteni wa timu ya Kurui yenye maskani yake Kata ya Mzenga amesema Kisarawe wajiandae watakapokutana kwenye mechi ya marudiano sababu lengo lao ni kucheza fainali na si vinginevyo.
Diwani wa Kurui Mhe.Mussa Ruhikuni amesema kuwa michuano hii inakuza uhusiano miongoni mwa Kata za Kisarawe pia kwa niaba ya wananchi anamshukuru Mhe.Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe kwa kupitia michuano ya Jafo Cup vijana wameepukana na kujiunga na makundi yasiyofaa.
Diwani wa Kata ya Kisarawe Abel Mudo amesema kuwa michuano hii inaleta burudani huku amesifu mechi ilivyokua ya kuvutia kwa sababu timu zote zinaonekana zimejiandaa vya kutosha .
“Nawapongeza waandaaji wa Jafo Cup kwa sababu wananchi wetu wamefurahia na kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huu pongezi kwa Mh.Jafo kwa kuja na wazo hili la kuwakutanisha vijana wa rika zote michuano hii iendelee” amesema Mh.Diwani Abel.
Kocha wa timu ya Kisarawe Maliki Hilali Dachi amewaahidi ushindi wa kishindo mashabiki wa Kisarawe FC kwenye mechi yao ya marudiano na kusisi ushindi utakuwa kwao na watabana ipasavyo Kurui FC.
Kocha wa Kurui FC Fikiri Kikondo amesema kuwa wao hawajawahi kushindwa kwenye michezo yote ya nyumbani na ugenini hivyo Kisarawe FC wajipange tena watakapokutana nao Januari 25 mwaka huu
Michuano ya Jafo Cup imeanza Juni 2024 imeshirikisha timu kutoka Kata zote 17 na Vijiji 65
Mshindi wa Jafo Cup ataondoka na done nono kiasi cha Mil.2 pamoja na pikipiki mbili huku mshindi wa pili ataondoka na Mil.1 pamoja na pikipiki fainali hiyo itachezwa Manerumango Kisarawe Pwani.