MSHAMBULIAJI wa zamani wa Mlandege FC ya Zanzibar, Oscar Evalisto amejiunga na Makadi FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, Misri.
Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye kikosi cha Mlandege kilichoifunga bao 1-0 Simba, kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup msimu uliopita.
Makadi msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya sita kati ya 10 baada ya michezo 28, ikishinda mitano, sare 12 na kupoteza 11 na kukusanya pointi 27.
Mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia Mwanaspoti nyota huyo tayari amesaini mkataba na yuko njiani kwenda Misri.
“Amesaini mkataba wa miezi sita wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja kama atafanya vizuri, hii ni fursa kwake kama ataonyesha kiwango bora,” alisema mtu huyo.