Mkutano Mkuu CCM wataka Rais Samia, Dk Mwinyi wagombee 2025

Dodoma. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania urais.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts