KIUNGO wa Zed FC inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Misri, Maimuna Hamis ‘Mynaco’ alisema ni mara ya kwanza kucheza na Al Ahly na anatamani timu yake ipate ushindi.
Mtanzania huyo ni msimu wa pili kucheza katika ligi hiyo akisajiliwa kutokea Yanga Princess ambako alicheza kwa msimu mmoja 2022/23.
Akizungumza na Nje ya Bongo, Mynaco alisema huo ni mchezo wa kwanza kucheza dhidi ya Al Ahly ambayo ndiyo msimu wake wa kwanza kushiriki ligi hiyo.
“Ni mchezo mgumu sana kwa upande wetu, hii ni mara ya kwanza tunakutana, natumai hautakuwa mwepesi kwetu kwa sababu pia tunahitaji pointi tatu,” alisema Mynaco.
Alisema Kuhusu kiwango chake msimu huu atapambana na anamtanguliza Mungu kwenye kupata mafanikio; “Kupambana ni jukumu letu, kufanikiwa ni kazi ya Mungu tusubiri muda utaongea.”