Na Said Mwishehe,Michuzi TV
NILIKUWA Najiongelesha tu kichwani kuhusu hii CCM basi nikajikuta nacheka tu,ndio kununa siwezi. CCM kwa jinsi walivyo hawa watu wanaakili mingi sana yaaani,mi nakwambia weee kunja sura ila haitakusaidia zaidi ya kujizeesha tu.
Wakati wewe unaiangalia leo na kesho kumbe wenzio wanaingalia mbele zaidi yako.Ukiwa wewe unaitazama Januari basi CCM wanaitazama Desemba. Wanajua sana kupanga mambo yao na ukiwa nyuma ya muda watakuacha halafu wenzio walee na kamziki kwa mbaaaali Iyena Iyena CCM nambari One.
Wakati unajipanga kwa ajili ya kuiuliza CCM kuhusu mambo yake kumbe yenyewe ilishakuwa na majibu yake kitamboooo halafu wanakaa kimya wanasubiri.
Kwa mfano wakati wewe unajipanga kuwauliza nani atakuwa mgombea urais wao katika uchaguzi mkuu 2025 kumbe wenyewe tayari jibu wanalo ni Samia Suluhu Hassan udongo kutoka aridhi ya Kizimkazi.
Wakati unajiuliza nani atakuwa Mgombea mwenza Dk.Samia Suluhu Hassan anakuja na jibu halafu anatoa jina akiwa amelilaksi tu kwamba namleta kijana wetu Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi. Wako shapu sana katika kuweka mipango,kusuka mikakati yao ndio maana unaona mambo yao yanawanyookea.
Chama kinawazee muda wote kinakwamaje? Si umeona juzi Rais mstaafu Jakaya Kikwete alivyowakilisha wazee wenzake katika ishu ya jina la mgombea urais.Wajumbe wa mkutano mkuu maalum walianzisha hoja ya kutaka Rais Dk.Samia Suluhu Hassan mitano tena.
Pia wajumbe wa mkutano mkuu maalum ambako kikatiba wakataka na Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kule Zanzibar naye mitano tena. Wajumbe wanatoa hoja,wanatoa sababu kwanini Samia na Hussein Mitano tena halafu wakiona kama huelewi wanachozungumza wanakutajia miradi ya maendeleo iliyofanywa na Dk.Samia na Dk.Mwinyi. Hapo lazima ukubaliane na hoja zao,mi mwenyewe wameshanikamata tayari yaani kwa uchaguzi mkuu mwaka huu ni Samia,ni Mwinyi.Ndio hivyo tena.
Wakati hoja ya Dk.Samia na Dk.Mwinyi wapewe mitano tena wajumbe wa mkutano mkuu maalum uliofanyika Januari 19,2024 walikuwa na mzuka yaani fulu vaibu. Halafu anatokea Jakaya mzee wa Msoga anawaambia vijana tulieni kwanza halafu tukishaamua mtashika mabango halafu anatoa hoja kisha anaanzisha wimbo wa Tunaimani na Samia halafu wajumbe wanaitikia kweli kweli Samia.
Wanapitisha Azimio kwa asilimia 100 kwamba 2025 ni Dk.Samia,ni Dk.Mwinyi uchaguzi 2025 halafu wanakuja na mgombea mwenza Dk.Nchimbi Wee unamashaka na Nchimbi ? Acha kujishaua. Kama humjui sema tukwambia kuhusu Nchimbi, kwa kifupi ametimia kila idara,anajua CCM inataka nini na Watanzania wanataka nini.Ngoja tusubiri Oktoba kubwa tuombeane uzima tu.
Ninaposema CCM wanajua kujibu maswali yao kabla ya kuulizwa uwe unaelewa mtu wangu,acha kujitoa ufahamu.Yaani Januari tu tayari wameshajua nani mgombea urais,nani mgombea mwenza wakati upande wa wapinzani wao wanavuana nguo hadharani kwa kurushiana tuhuma nzito nzito kisa nani atakuwa Mwenyekiti wa Chama kati ya Broo na Blaza.Patamu hapo.
Halafu ndugu yangu sio unakunja sura hapa napiga stori tu kama nakuboa achana nayo ila ukumbuke tu CCM noma sana.Wanasuka mipango yao wakati wengine wakiwa wamelala. Watu wamenda Dodoma katika Mkutano Mkuu maalum kupitisha jina la Makamu Mwenyekiti lakini wanamaliza mkutano tayari wana majibu ya kuelekea Oktoba kwenye uchaguzi mkuu.
Unajenga hoja inaungwa mkono wala hakuna kunyooshana kidole. CCM nyie kweli mnapotaka jambo lenu hamshindwi.Nimewavulia kofia… Ujue nilikuwa Dodoma na nilibahatika kushiriki mkutano mkuu maalum kwa kualikwa, nilikuwa nawaangalia wajumbe wanavyojenga hoja mbalimbali lakini katika hoja ya mgombea urais hapo nimepata somo jingine CCM inawatu asikwambie mtu kila anayesimama moto iwe kijana ,iwe mzee ni moto.
Kwa lugha rahisi CCM ina kila kitu, ukitaka waliosoma wapo wa kutosha wapo na ukitaka wasiojua kusoma nao wapo lakini kila mtu anakazi yake kwa wakati wake ni suala muda.
Halafu wenyewe wanakipenda Chama chao ,unawatukana ,unawasimanga wanakuangalia tu lakini linapokuja suala la uchaguzi ndio utajua wako siriazi kiasi gani.
Sasa tufanye hivi tufunge mjadala lakini nikukumbushe tu 2025 ni Samia,ni Mwinyi halafu mgombea mwenza Dk.Nchimbi. Hadi rahaa.Ukiichukulia poa CCM ujue itakula kwako halafu baada ya uchaguzi ndio unakuja kukumbuka KUMBE UBAYA UBWELA.
Kasimu kangu 0713833822.