Rais wa Moët Hennessy wa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, Atembelea Duka la Msanii Jux

Moët Hennessy inaendelea kuthibitisha uwepo wake kwenye soko linalokua la Tanzania ambapo Thomas Mulliez, Rais wa Moët Hennessy kwa Ulaya, Mashariki ya Kati, na Afrika, amezuru nchini Tanzania. Ziara hiyo muhimu imeangazia kuongeza imani ya kampuni hiyo ya kimataifa yenye vinywaji bora kabisa duniani nchini Tanzania kama sehemu inayokuwa kwa kasi na inasisitiza dhamira yake ya kukuza ukuaji wa uchumi katika kanda.

Katika ziara yake, Thomas Mulliez alichukua muda kuzungumza na watu maarufu wa Tanzania, akiwemo Juma Jux, msanii maarufu na mjasiriamali. Wawili hao walikutana kwenye duka kubwa la Jux African Boy lililopo Sinza, ambapo Mulliez alitembelea duka hilo na kufanya mazungumzo na Juma Jux. Mkutano huo ulihusisha kusherehekea michango ya Juma Jux kama ishara ya kuunganisha maadili ya Hennessy na utamaduni wa Kiafrika.

Juma Jux, msanii wa muziki anawakilisha ushirikiano mzuri kati ya Hennessy na Sanaa za Kiafrika. Kupitia ushirikiano wake na Hennessy, Juma Jux ameonyesha dhamira ya chapa hiyo kusherehekea vipaji vya Kiafrika kwenye jukwaa la kimataifa. Hasa, alishiriki katika shuguli mbalimbali kama vile Michezo ya NBA huko Paris mnamo mwaka 2023 na Ligi ya Kikapu ya Rwanda ya Afrika mnamo 2024, ikionyesha uhusiano wa kina wa Hennessy kwa michezo na utamaduni wa Kiafrika. Akizungumza juu ya mkutano huo, Thomas Mulliez alielezea kufurahishwa kwake na mafanikio ya Juma Jux: “Juma Jux anaonyesha kuuhisi ubora na ubunifu ambayo ama kwa hakika inalingana na maadili ya Hennessy. Mafanikio yake nchini Tanzania na kwingineko ni uthibitisho wa nguvu ya ushirikiano baina yetu.”

Juma Jux alitoa shukrani zake kwa kusema, “Ni heshima kushirikiana na Hennessy, chapa ambayo sio tu inatambua na kuibua vipaji vya Kiafrika. Ushirikiano wetu pia unajumuisha kusherehekea vipaji vya Watanzania na umoja wa kimataifa.”

Uwepo wa Moët Hennessy nchini Tanzania ni kielelezo cha maono mapana ya kampuni hiyo kukuza masoko yanayoibukia huku ikikuza ushirikiano. Ziara ya Mulliez pia imetumika kama fursa ya kuimarisha ushirikiano, kutafuta fursa za ukuaji, na kusherehekea mambo mbalimbali.

Ziara hii inaonyesha juhudi zinazoendelea za Moët Hennessy za kuiweka Tanzania kama soko madhubuti la biashara yake maarufu duniani ya mvinyo na vinywaji vikali huku ikisherehekea mafanikio yake.

Related Posts