Waziri wa Afya Mhe Jenista Mhagama atoa Rai kwa Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kuangalia namna bora itakayowezesha mfuko kutatua changamoto zote za upatikanaji wa vifaa tiba kwa haraka kwa kushirikiana na wadau ili wanachama wa mfuko huo wasighadhibike kwa namna yeyote wanapohitaji huduma bora kutoka kwenye vituo vya Afya.
Waziri Mhagama ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Januari 21,2025 wakati Akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Na kuongeza kuwa matamanio yake ni kuwa zile huduma zote za msingi zipatikane kwenye Bima ya Afya kwa wote.
“Sasa niendelee kutoa Rai kwa wajumbe wa Bodi kuangalia namna bora itakayowezesha mfuko kuhakikisha changazote zinazotokana na upatikanaji wa vifaa tiba zinatatuliwa kwa haraka sana kwa kushirikiana na wadau watoa huduma za afya ili wanachama wetu wasighadhibike kwa namna yeyote wanapohitaji huduma zilizo bora kutoka kwenye vituo vyetu wanavyotolea huduma za afya”.
Aidha Waziri huyo ametoa Maagizo mengine kwa uongozi wa mfuko huo ikiwemo kuhakikisha mapato ya mfuko yanatumika vizuri kwa kazi zinazotambulika,Kufanya kazi kwa karibu na sekta Binafsi ili kusaidia kuingeza juhudi kwenye Sekta ya Afya na pia kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu vifurushi walivyokubaliana na vinavyofanya kazi kwenye Bima ya Afya kwa wote.
“Sasa nitoe maagizo machache ya kuwa Hakikisheni mafanikio haya ambayo yamefanya mfuko kuwa na ziada ya mapato,mapato yanatumika vizuri kwa kazi zinazotambulika na kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na matumizi halisi ya mapato ambayo tumejipatia”.
“Eneo lingine Niendelee kuwakumbusha kufanya kazi kwa karibu na Sekta binafsi,kwasababu tunaichukulia kama sekta itakayosaidia kuongeza juhudi kwenye sekta ya afya na sio kuwa chukulia kama washindani kati ya sekta za Umma na sekta binafsi,kwani zipo Hospital kubwa za sekta binafsi zinazofanya vizuri na kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya,hivyo kushirikiana nao”.
“Eneo lingine ni kuhakikisha vifurushi vile ambavyo tulikubaliana na vinafanya kazi vinaendelea kutolewa elimu na kusomamiwa vizuri ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi”.
Awali akitoa salamu Dkt Baghayo Saqware ambaye ni Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ameleeza kuwa wanufaika wa Bima za afya na bima zingine wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2021 wanufaika walikuwa milioni 14.2 na mwaka 2022 milioni 17.8 huku mwaka 2023 walifikia milioni 23 sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 29 kila mwaka.
“Ukijumlisha bima za afya na bima zingine wanufaika wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka, mwaka 2021 tulikuwa na wanufaika milioni 14.2 wakati mwaka 2022 walikuwa milioni 17.8 na mwaka 2023 wamefikia milioni 23, hili ni ongezeko la wastani wa asilimia 29 kwa mwaka na hii inatokana na Sera nzuri na maelekezo mazuri kutoka kwenye Wizara zetu za kisekta na Wizara ya afya”.
Kwa upande wake Dkt Irene Isaka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF) mbali na kueleza mafanikio ya Bodi iliyomaliza muda wake kuwa waliweza kuongeza wigo wa wanufaika wa bima afya kwa kusimamia usajili wa wanachama lakini amekili kuwa walikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa gharama za magonjwa yasiyoambukiza, Uhiari wa wananchi kjiunga kwenye mfuko wa bima ya afya na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa rufaa ya wagonjwa nchini.
“Bodi iliyomaliza muda wake ilikuwa na changamoto kadhaa,moja wapo ni kuongezeka kwa gharama za magonjwa yasiyoambukiza,kukosekana na utamaduni kuwa na bjma kwa wananchi kabla ya kujiunga, Uhiari wa wananchi kujiunga kwenye mfuko wa bima ya afya,kuchelewa kulipwa kwa fedha ambazo mfuko uliikopesha Seeikali,Kukosekana kwa mfumo madhubuti wa rufaa ya wagonjwa nchini”.
“Vile vile walifanikiwa kuongeza wigo wa wanufaika wa Bima ya Afya kwa kusimamia usajili wa wanachama ambapo walitoka milioni 1,212,519 mwaka 2020 hadi kufikia milioni 1,246,046 machi 2024 sawa na ongezeko la asilimia 3”.
Bodi hii iliyozinduliwa leo na Mhe Waziri wa Afya Mhe Jenista Mhagama ni Bodi ya 6 tangu kuanza kwa Bodi za Mfuko huu.