Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amemteua John Mnyika kuendelea kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema, nafasi aliyokuwa akiishikilia tangu Freeman Mbowe alipokuwa mwenyekiti.
Pia Lissu amemteua Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Salum Mwalimu aliyeondolewa.
Amani Golugwa aliyekuwa ‘campaign manager’ wa Lissu katika uchaguzi mkuu wa 2020, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Benson Kigaila ambaye naye ameondolewa.