TUNDU LISSU ASHINDA UWENYEKITI CHADEMA, MBOWE ABARIKI MATOKEO

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TUNDU Lissu ameibuka mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) dhidi ya mpinzani wake ambaye mtangulizi wake, Freeman Mbowe aliyekuwa anatetea nafasi yake.

Katika ukurasa wake wa Mtandao kijamii wa X, Mbowe ameandika ujumbe wa kukubali kushindwa kwa kusema “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya Uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama”,

Mbowe ameikiongoza Chama tangu alipochaguliwa nafasi hiyo mwaka 2004 akirithi mikoba ya Bob Makani aliyeongoza chama hicho kuanzia mwaka 1999. Tundu Lissu nae amekuwa kwenye Chama hicho kwa zaidi ya miaka 20 huku akishika nafsi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama ambapo kabla ya uchaguzi huu alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Related Posts