FEZA Boys yafaulisha wanafunzi wote

SHULE Sekondari Feza Boys imejivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi kuwa bora baada ya kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja la kwanza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulifanyika mwaka 2024, huku zaidi ya asilimia 65 wakipata division 1.7.

Hayo ameyasema Makamu Mkuu wa Shule ya FEZA Boys, Shabani Mbonde wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2025 katika shule hiyo iliyopo Kunduchi Dar es Salaam mara baada ya Baraza la Mitihani kutangaza matokeo ya kidato cha nne.

Mbone ameleeza kuwa matokeo hayo hajatokea tu kirahisi bali ni uwekezaji na mazingira ya shule yanayomtengeza mwanafunzi kuwa bora na walimu wa kutosha ambapo kila mwalimu ana wastani ya kufundisha wanafunzi 10.

” FEZA SHOOLS haitoi mwanafunzi bora katika A tu, bali katika nyanja zote.Sisi katika elimu hatumjengi mwanafunzi kupata A tu lakini pia katika kukabiliana na hali zote katika maisha kulingana na wakati uliopo.

“Hii yote inatokana na jitihada mbalimbali za wanafunzi wenyewe na walimu. Mwanafunzi wetu anakuwa ni kama ametoka kwenye mashine au kiwanda kilichomjenga katika kupambana na changamoto mbalimbali katika mtihani na maisha.Tunajivunia wanafunzi wetu na walimu wetu,” amesema Makamu Mkuu huyo.

Aidha Mbonde amesema kama sekta binafsi wanashukuru serikali kwa kusisitiza suala la elimu na wanaiunga mkono Serikali katika kuhakikisha elimu inakuwa bora.

Naye Mkuu wa taaluma msaidizi wa kidato cha tatu na nne, Abdallah Juma ameeleza mbinu wanazotumia kuwafundisha wanafunzi hao kuwa ni progamu mbalimbali walizonazo shuleni hapo.

” Sio kwamba sisi vijana wote tunaowachukua ni wale ‘cream’ tu bali wanakuja hata wenye uwezo mdogo tunawatengeneza na wanakiwa sawa na wenzao na wanafaulu kwa pamoja.

” Matokeo haya yamepatikana kwa njia tofauti, pande zote tatu zina mchango yaani wazazi, walimu na wanafunzi, pia tuna programu mbalimbali za masomo kuanzia asubuhi, jioni na hata usiku, pia wanapata muda wa kucheza”, amesema.

Kwa upande mmoja wa wanafunzi wa FEZA BOYS waliofanya vizuri kwa kupata division one 1.7, Moses Francis, amesema anamshukuru Mungu kwani mafanikio hayo hayakuja kirahisi ya kupata A masomo yote 10 ila mazingira ya shule yamechangia ikiwamo kusoma kwa bidii kama mwanafunzi.

Amefafanua kuwa kutokana na ratiba za shule zilivyopangiliwa wanapata muda wa kutosha wa kupumzika lakini kuna kipindi kigumu unatakiwa kusoma sana ili kufaulu mtihani.

“Hii haipatikani kirahisi, mtu kufaulu lazima kuwe na motisha kuanzia kwa mwanafunzi wenyewe na mzingira mazuri ya kujifunzia pamoja na kumtanguliza Mungu.Kila wiki tunafanya mazoezi ya masomo kwa kufanya test,” amesema Moses.

Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ufaulu umeongezeka ambapo jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo sawa na asilimia 92.32 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I,II,III,IV.

Makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Feza Boys ,Shabani Mbonde akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa matokeo ya kidato cha nne na shule hiyo kupata ufaulu wa alama A kwa wanafunzi waoote kwenye atokeo ya kidato cha nne.Kulia ni mmoja ya mwanafunzi aliyepata ufaulu wa A. Mosses Mwaijande na Kushoto ni Mtaalumu Abdalla Juma

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Allan Masaka aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A .Na,mpiga picha maalumu

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Moses Mwaijande aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A .Na,mpiga picha maalumu
 

Related Posts