NDANI ya kikosi cha Simba mtambo wa kutengeneza mabao ni Jean Ahoua ambaye haeleweki kutokana na kiwango chake kuwa cha kupwa na kujaa lakini ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Ipo wazi kwamba Simba kwenye ligi ni namba moja katika msimamo ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 15 ni namba mbili kwa timu iliyofunga mabao mengi ambayo ni 31 ikiwa namba moja kwa timu iliyofungwa mabao machache ambayo ni matano.
Jean Ahoua ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu kwenye kikosi hicho akiwa ni mchezaji mwenye bahati, huku uongozi ukibainisha kuwa bado hajafikia ubora wa asilimia 100 ndani ya uwanja.
Ahmed Ally, Meneja Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua uwezo wa Ahoua hivyo bado ataendelea kuwa bora zaidi kwenye mechi zijazo ili kuwapa furaha Wanasimba.
“Unajua Ahoua bado hajafikia asilimia 100 za ubora wake, taratibu anazidi kuimarika licha ya kwamba anafunga bado, huwezi kumuelewa Ahoua hana mambo mengi utamkuta kwenye furaha tayari kafanya yake.”
Ahoua ni mkali wa mguu wa kulia ambapo mabao yake yote 7 aliyofunga ndani ya ligi ametumia mguu huo. Katoa pasi 5 hivyo kahusika kwenye mabao 12 ndani ya kikosi cha Simba ambacho kimefunga mabao 31.
Ahoua ni mkali kwa mapigo ya penalti akiwa amefunga mabao matatu kwa penalti. Mbali na mapigo ya penalti kwenye mapigo ya faulo yaani free kick yupo alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar akiwa nje ya 18.
Sio nje ya 18 ama ndani ya 18 Ahoua nim kali kwenye kutupia ambapo katupia mabao matano akiwa ndani ya 18 na mabao mawili kafunga akiwa nje ya 18.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.