Nchimbi avunja ukimya ishu ya pete

MSHAMBULIAJI wa Mbeya Kwanza, Ditram Nchimbi ameamua kuvunja ukimya juu ya kusakamwa mitandaoni kutokana na video inayomuonyesha akimvisha mwanamke pete ya uchumba, huku akiweka bayana sakata zima la mkewe.

Alifafanua ishu ya video aliyekuwa anamvalisha mwanamke pete aliyeonekana kumzidi umri, akisema ni video ya zamani, huku zikiwepo taarifa za chinichini za kumuacha na mkewe, kipindi hicho alikuwa anacheza Yanga.

“Wapo waliosema mwanamke ni mkubwa nimefuata pesa ila jibu langu ni upendo ni hisia za mtu na sio kuchaguliwa niwe na nani, kuna wengine walisema nimemvalishia pete baa, hapana ilikuwa ni nyumbani na zile video waliposti wageni waalikwa na sio mimi,” alisema Nchimbi na kuongeza;

“Nilikaa bila mahusiano baada ya kuachana na mke wangu mwaka mzima, hivyo nisahihishe shutuma hizo, sikumwacha mke wangu na kwenda kwa mwingine na huyo niliyemvisha pete tulishaachana kwa sasa nina mtu wangu mwingine.”

Nchimbi aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali kama Maji Maji, Mbeya City, Njombe Mji, Azam FC, Polisi Tanzania, Yanga, Geita Gold na Etincelles ya Rwanda, alisema kila anachokifanya katika maisha yake kipo kwa ajili ya kumfurahisha na sio kuwapendezesha watu.

Related Posts