WANAHARAKATI, WANAZUONI WASEMA UISLAMU SIO KIKWAZO MWANAMKE KUWA KIONGOZI

Na Nihifadhi Abdulla, Zanzibar.

ZANZIBAR ni moja kati ya nchi ambayo inadaiwa kuwa na waumini wa kiislam wengi na huishi kwa kufuata sunna, vitabu vitukufu, na historia za viongozi wa dini wa zama zilizopita lengo ni kujenga imani iliyo ya kweli kwakufuata misingi na taratibu zinazoonekanwa ni sahihi.

Suala linalohusu hadhi ya mwanamke katika jamii limekuwa likizusha mijadala juu ya ushiriki wake katika ngazi za maamuzi, zipo tamaduni zinaunga mkono na nyengine zinapinga suala hilo kwa kunasibisha na Dini ya Uislam.

Ukhty Amina Salum mwanaharakatina mwanazuoni ameeleza Chanzo kikuu cha kutokezea rai hizo mbili ni kuwepo mitazamo tofauti juu ya suala zima la mwanamke kuruhusiwa ushiriki katika utowaji ya maamuzi, jamii na kitaifa au haruhusiwi”hii inakuja kwa vile jamii haijawa tayari kujifunza kiundani bali huamini maneno ya kuambiwa lazima mtu ajifunze maana hata wakati wa mitume wanawakewalikuwepo ambao ni viongozi na walionekanwa wakifanya kazi nzuri,

“Jamii inapaswa kuhamasika kuachana na dhana potofu juu ya uwezo wa mwanammke na maamrisho ya dini kuhusiana na wanawake kushiriki katika uongozi”amesisitiza Ukhty Amina.

Katiba ya Zanzibar kifungu cha 21.(1) kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu mwanamke na taifa, mbali na hayo kuna matamko mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ambayo imekuja kutetea haki za wanawake ikiwemo mkataba wa CEDAW, SADC, azimio la 1325 la usalama la umoja wa Mataifa.

Profesa Issa Ziddy Mhadhir kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA anasema Historia ya uislam ina mifano hai inayoonesha kuwa kuna maeneo mengi ambayo waislamu wanawake wamewapiku/wamewashinda wanaume katika ushiriki wao kwenye ngazi mbalimbali zinazopelekea kutolewa maamuzi ya busara na kupatikana ushindi “mfano mzuri ni wa bi balqis ambae alikua mkuu wa nchi inayosemekana kwasasa ni yemen aliwaongoza vyema watu wake mpaka akawaepusha na vita ambavo baadhi ya viongozi wanaume walikua wanashadidia vitokee,

Kitabu cha Qur-an kinaeleza dini ya kiislam ilivomtukuza na kumfadhilisha binaadam wa kike na kiume kuliko viumbe wote duniani surat Israa: aya ya 70 hii inamaana ya kwamba haijabagua kati ya mwanamke na mwanamme na wote kupewa hadhi sawa”anasema Profesa

Kuna fat-wa za baadhi ya maulamaa wakubwa akiwemo mufti mkuu wa misri Dkt Shauqy Alaam mnamo mwezi wa 8 2018 alipojibu kuwa inafaa mwanamke kuwa rais wa nchi, na ndio maana kuna baadhi ya nchi zenye waislam wengi ambazo marais au mawaziri wakuu ni wanawake ikiwemo Pakistan, Senegal, Bangladesh nk.

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika kifungu cha 25 ibara ndogo ya kwanza kimeeleza kuwa kila mtu anawajibu wa kupata haki zake za lazima na uhuru binafsi bila kujali kabila,pahala alipotoka au maskani au mahusiano mengine yoyote yale

Inadaiwa kuwa ingawa si kwa kiasi kikubwa kama zamani bado jamii inaimani mwanamke hawezi na hafai kuwa kiongozikwa kutumia kizingiti cha dini huku wakitoa hoja zao lukuki ambazo tayari zimeshatolewa ufafanuzi na wanazuoni mbalimbali.

Katika kuhakikisha wanawake wanapata haki yao ya kuwa viongozi jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali bali hata taasisi binafsi, Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar ni miongoni mwa taasisi iliyo mstari wa mbele kupambania haki ya mwanamke Sabrina Mwintanga Afisa Mradi TAMWA wa kuwainua wanawake kwenye uongozi (SWILL) anaeleza katika kuwaandaa wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi hutumia viongozi wa Dini kuengeza nguvu ya ufahahamu kwa jamii.

“TAMWA tumejipanga kuelekea uchaguzi wa 2025, tumelenga kuongeza idadi ya wanawake katika ngazi za maamuzi visiwani Zanzibar katika harakati zetu tunashirikiana sana na viongozi wa dini kwani wanafanya kazi kubwa kueleimisha jamii na ikafahamu na tunaona imezaa matunda kwani sasa hivi tofauti na zamani mwanamke alikuwa hawezi hata kuzungumza sehemu ambayo kuna wanaume,

Licha ya hayo Sabrina ametoa rai kwa kusema “ni vyema wanawake kutowekewa vizuwizi na mipaka katika kugombea nafasi za kuingia kwenye vyombo vya kutowa maamuzi kwa kisingizio cha dini bali wapewe fursa za kujiongezea elimu ili washiriki kwa weledi kushika nafasi za uongozi”amemalizia Sabrina

Dadi kombo amesema awali alikua miongoni mwa watu ambao hawaoni umuhimu wa mwanamke kuwa kiongozi na aliamini kazi ya mwanamke ni kulea familia na kusimamia majukumu ya nyumbani “ baada ya kupata elimu kutoka TAMWA nimekuwa balozi kwa wenzangu na sasa mimi ni Mwanammewa mabadiliko,

Mradi wa kawawezesha wanawake kwenye uongozi (SWILL) unaotekelezwa na TAMWA- ZNZ kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) kwa mashirikiano makubwa na Ubalozi wa Norway ni wa miaka mitatu kuanzia 2024 2027 una lenga kuwainua wanawake na wasichana kupitia nyaja mbalimbali na kufikia usawa wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi.

Related Posts