TANZANIA NCHI YA MFANO USAWA WA KIJINSIA

Na Pamela Mollel,Arusha 

Tanzania imeendelea kuwa nchi ya mfano katika kukuza usawa wa kijinsia, hasa kwa hatua zake za kihistoria za kuwa na Rais mwanamke wa kwanza, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Aidha, uwakilishi wa wanawake bungeni umefikia asilimia 37, hatua inayoashiria maendeleo makubwa katika kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye uongozi na maamuzi ya kitaifa.

Hayo yamesemwa leo Januari 23,2025 jijini Arusha na mwakilishi wa Nchi UN Women Bi.Hodan Addou akifungua mafunzo ya siku tatu ya Uongozi kwa wanawake viongozi kwenye ngazi ya serikali za mitaa

“Napongeza sanaa Tanzania kwa kufikia hatua hii kwa kuwa na viongozi wanawake ni mfano tosha katika kukuza usawa wa kijinsia “anasema Bi.Addou

Katika mafunzo hayo zaidi ya wanawake mia sita  kutoka Mikoa saba wanatarajiwa kujengewa uwezo kuhusu maswala ya  uongozi na ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi .

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka idara ya sayansi ya siasa  na utawala kutoka chuo kikuu cha DSM ,Prof.Bernadeta Killian anasema kuwa,wanatoa mafunzo hayo kwa  viongozi wakiwemo madiwani waliochaguliwa, madiwani wa viti maalum,wenyeviti wa serikali za mitaa na wenyeviti wa serikali ya kijiji ,pamoja na wenyeviti wa majukwaa mbalimbali mkoani Arusha .

Mafunzo hayo ambayo ni  ya mradi wa mwaka mmoja  yamefadhiliwa na shirika la UN Women Tanzania kwa kushirikiana na serikali  ya finland








Related Posts