TUZO za TEHAMA 2025 zimelenga kutambua mchango mkubwa katika sekta ya TEHAMA ya Tanzania, kwa kuwatambua watu binafsi, mashirika, na miradi inayochochea mabadiliko ya kidigitali, kuimarisha ubunifu, na kukuza ushirikishwaji.
Ameyasema hayo leo Januari 24, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tuzo za TEHAMA 2025 ambazo zitafanyika Februari 21, 2025 Jijini Arusha.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Amesema hafla hiyo itakuwa jukwaa muhimu kwa viongozi wa sekta, watunga sera, na wabunifu kushirikiana, kuungana, na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kidigitali nchini.
Aidha Dkt. Mwasaga amewahimiza Wabunifu, Wadau wa TEHAMA, startups, taasisi za sekta ya umma na binafsi, na mashirika yote Tanzania kushiriki kwenye tuzo za mwaka huu kwa kuwasilisha uteuzi wao katika vipengele kama vile, Ubunifu katika Bidhaa au Huduma za TEHAMA, Matumizi Bora ya TEHAMA, TEHAMA kwa Maendeleo ya Jamii, Kijana Aliyefanikiwa Katika TEHAMA, Wanawake Katika TEHAMA, Usalama wa TEHAMA, Mradi wa TEHAMA wa Sekta ya Umma, TEHAMA Endelevu, Tuzo za TISPA kwa Mtoa Huduma Bora ya Uunganishaji wa Mtandao,Tuzo Maalum ya Maisha kwa Mchango wa TEHAMA kutoka Wizara ya Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari.
“Kwa jumla ya tuzo 22 zinazotolewa, kila moja ya kipengele kilichoorodheshwa kina beba idadi ya vipengele vidogo vinavyowakilisha sekta na tasnia mbalimbali”. Amesema
Amesema mbunifu yeyote anaweza kujisajili au kumsajilia mtu ambaye unamfahamu kuwa ni mbunifu na wataalamu watachakata na mwisho kuweza kutambuliwa siku ya Tuzo hizo. Na tarehe ya mwisho ya usajili ni Februari 10, 2025.
Pamoja na hayo amewakaribisha wadau mbalimbali na wawekezaji kujumuika pamoja katika Tuzo hizo.
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Kampuni ya SoftVentures, ambao walileta wazo la Tuzo hizo, Daniel Mhina amesema wanafurahi kuaminiwa na Wizara kupitia Tume ya TEHAMA katika ushirikiano huo wa kuandaa Tuzo za TEHAMA 2025.
Amesema wanaahidi kuhakikisha Tuzo za TEHAMA kuwa za kipikee na endelevu ili miaka mingine iwe nzuri zaidi.
Nae Afisa Miundombinu TISPA, Joseph Rwegoshora amesema kuwa TISPA ni chombo cha sekta kinacho wakilisha watoa huduma za mtandao na wadau wa TEHAMA. TISPA inatetea ushirikishwaji wa kidigitali, maendeleo ya sera, na upanuzi wa miundombinu ya TEHAMA ili kusaidia ukuaji wa uchumi wa kidigitali nchini Tanzania.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2025 katika uzinduzi wa Tuzo za TEHAMA 2025 ambazo zitafanyika Februari 21, 2025 Jijini Arusha.

Afisa Miundombinu TISPA, Joseph Rwegoshora akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2025 katika uzinduzi wa Tuzo za TEHAMA 2025 ambazo zitafanyika Februari 21, 2025 Jijini Arusha.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Mwanzilishi wa Kampuni ya SoftVentures, Daniel Mhina akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2025 katika uzinduzi wa Tuzo za TEHAMA 2025 ambazo zitafanyika Februari 21, 2025 Jijini Arusha.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa Tuzo za TEHAMA 2025 ambazo zitafanyika Februari 21, 2025 Jijini Arusha.
Tuzo hizo zimezinduliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume ya TEHAMA nchini kwa kushirikiana na SoftVentures pamoja na Chama cha Watoa Huduma za Mtandao Tanzania (TISPA).
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)