Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 24, 2025 kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Hai.
KABLA ya kuhamishwa wilaya ya Hai, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko leo Januari 24, 2025 Mchana alizindua kampeni ya “Ubungo Usiku kama Mchana” ambapo katika wilaya hiyo kazi za uzalishaji na Shughuli za biashara zitafanyika usiku na mchana kwa siku saba za wiki kwa kila mwezi na kwa mwaka mzima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua kampeni hiyo na kuzungumza na Viongozi mbalimbali wa serikali za mtaa na Kata pamoja na wafanyakazi kutoka idara zinazotoa huduma katika jamii, Mbomboko amesema kuwa Kampeni hiyo itaenda kuonesha taswira halisi ya wilaya ya Ubungo ambayo ni ya kimkakati na ni lango la jiji la Dar es Salaam.
“Ajenda hii tumeamua kuibeba kwa sababu Wilaya yetu ya Ubungo ni eneo la kimakakati ni eneo ambalo ndio lango la jiji na ni eneo ambalo ninaplay part kubwa sana katika biashara za mkoa wetu wa Dar es Salaam, tunayo masoko makubwa ya kimkakati tunazo Kituo kikubwa cha mabasi na daladala na tunayo masoko.” Amesema Bimboko
Ameeleza kuwa maeneo hayo mhimu yanawafanya waweze kuangali namna watu wanaweza kufanya biashara kwa masaa 24 kila siku.
Amesema kuwa kunamambo ya msingi yanatakiwa yafanyike ili biashara na shughuli za uzalishaji ziweze kufanyika kwa ufanisi zaidi.
Amesema Ulinzi na usalama lazima uimarishwe na kuhakikisha kuwa wanatoa mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na uhakika wa usalama wa mali zao na wafanyabiashara wenyewe.
Amesema kuwa wamehakikisha huduma zote mhimu zinaendelea kutolewa kwa saa 24 hii ni pamoja na huduma za afya, huduma nyingine za kijamii, kama maji na umeme upatikane kwa uhakika kwa saa zote 24 lakini pia kuwa na uhakika wa miundombinu kama barabara ziwe zinazofikika katika maeneo yote ya wilaya ya ubingo na kuwa na taa za barabarani zinazotoa mwanga ili ziweze kutafsiri kazi zinazofanywa usiku na mchana.
“Usiku ili uwe mchana ni lazima kuwe na mwanga watu wanapofanyia kazi.”
Amesema wilaya hiyo wanamkakati wa kuhakikisha masoko, stendi na maeneo ya kimkakati na huduma za kijamii zinapatikana masaa 24 na zinafata uhakika wa mwanga wa kutosha katika maeneo yote.
Akizungunzia maandalizi ya kampeni ya Usiku kama Mchana, Bomboko amesema yameshakamilika kwa asilimia 80, ndio maana wameanza kutoa taarifa kwa umma, na asilimia zilizobaki wanaendelea kuimarisha miundombinu ili kufanikisha kampeni hiyo kwa saa zote 24.
Amesema kuwa masoko yaliyoainishwa ni Soko la Mahakama ya Ndizi, mabibo, Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi, kituo cha daladala cha Mbezi mwisho na Soko la Kichinjia kuku la Shekilango, Manzese Baharesa, Sinza na Mlimani City.
Amesema kuwa asilimia hizo zilizobaki wanaendelea kuonesha maeneo mhimu kama msigani Maramba, soko la Kwa Beda na Mburahati.