DC Mapunda awasihi wananchi kuhudhuria maadhimisho wa wiki ya sheria, Jaji Maghimba aeleza Mafanikio ya Digitali

MKUU wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda, ametoa rai kwa Wananchi kufika kwabwingi katika viwanja vya mnazi mmoja kwa ajili ya kujifunza kuhusu utendaji kazi wa mahakama na mifumo mengine ya kisheria.

Mapunda amesema hayo leo januari25 ,2025 wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini ambapo kwa Dar es Salaam umefanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.

Mapunda amesisitiza umuhimu wa wananchi kujua namna ya kutafuta haki zao mahakamani lakini na mifumo ya utoaji haki .

“Niwaombe wananchi wa Dar es Salaam mfike hapa viwanja vya mnazi mmoja ni mara chache sana huduma hizi kuzipata bure”.

Amewasisihi maofisa wa mahakama waliokuwa kwenye mabanda ya maonyesho ya wiki ya sheria kutochoka kuwaelemisha wananchi kuhusu sheria.

“Mfanye kazi bila kuchoka maana huo msalaba ambao Mungu amewapatia kwa muda mfupi niliofanya kazi kama Mkuu wa Wilaya nimeona kazi yenu mmetusaidia sana kutatua migogoro ya ardhi imekuwa shida muda unapoamka unasikia migogoro ya ardhi mmetusaidia sana”, Amesema Mapunda.

Mapunda amewataka wananchi kuendelea kuitunza amani ili nchi iendelee kustawi.

“Tuanze na amani na utulivu kwenye ngazi ya familia amani na utulivu haipatikani kwenye mifarakano”, amesema Mapunda.

Pia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza na kujiandikisha kupiga kura pale tarehe zake zitakapotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi Mwaka huu.

Amesema kuwa mifumo ya utoaji haki imeimarika kiasi kwamba mahakimu au majaji wanaweza kusikiliza kesi kutokea sehemu yoyote nchi kwa mifumo ya kidigatali.

“Unaweza ukawa na Jaji mmoja yupo hapa Dar es Salaam akasikiliza mashahidi waliokuwepo Tandahimba na shughuli zikaenda na mahakama ikaenda vizuri ni kitu ambacho hakijawahi kutokea huko nyuma mahakama ilikuwa inaonekana haiamini kwenye teknolojia bali kwenye makaratasi”, amesema Mapunda.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salam, Jaji Salima Maghimbi amesema katika kuadhimisha wiki ya sheria nchini kutakuwa na mijadala itakayojadili kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ‘Tanzania ya mwaka 2050 nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai ‘

Anasema kuwa mahakama imejipanga kutekeleza kwa vitendo mpango wa maendeleo wa Taifa wa 2050 .

Jaji Maghimbi amesema kuwa mahakama itatoa taarifa ya utendaji kazi wake wa mipango yake mkakati inayotekelezwa kwa miaka mitano.

“Mwaka huu tutapata mrejesho kwa watumiaji wa huduma zetu ili tuweze kuutumia kwenye mpango wa 2025 “

Jaji Maghimba amesema siku ya tarehe 6 Novemba 2023 ilikuwa siku ya kihostoria ya Mahakama ilikuwa siku ya mahakama kuhama kutoka kwenye mifumo ya analojia kwenda kwenye mifumo ya kidigatali.

Amesema kuwa mageuzi hayo yameleta mafanikio makubwa katika mahakama ambapo kwa mwaka 2024 mashauri 37988 yalisajiliwa ambapo kati ya hayo mashauri 37953 yalisikilizwa na kufikia kiwango cha kuondoshwa kwa asilimia 100 hadi kufikia Desemba 2024 mashauri 7343 sawa na asilimia 8 ya mashauri yaliyobaki “tuliweza kuondoa mrundikano wa mashauri kwa asilimia 80 kutokana na kasi ya kusikiliza mashauri kwa njia ya kidigitali”

Jaji Maghimba amesema kuwa mbali na kutoa huduma za kisheria katika maadhimisho ya wiki ya sheria kutakuwa na bonanza na michezo mbalimbali kama vile Rede (Nage) Kukimbia na Gunia, kuvuta kamba, drafti , bao sambamba na uzinduzi rasmi wa Mahakama ya Mwanzo ya Wazo Hill tarehe 31 Januari.

Bendi ya Jeshi la Polisi ikiongoza matembezi kuelekea uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika Mkoa wa Dar es Salaam. Picha chini ni umati mkubwa wa Wananchi waliojitokeza kwenye matembezi hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sixtus Mapunda (kulia) akiwa na Majaji katika matembezi hayo. Mweye truck suit karibu yake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi.

Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania (juu na chini) wakikatiza mitaa ya jiji la Dar es Salaam.

Mabango ya Wadau mbalimbali wa Mahakama ambayo yamebeba ujumbe mkuu wa Wiki na Siku ya Sheria. Picha chini ni Kikundi cha ‘Jogging’ kikianikiza katika matembezi hayo.

Ulikuwa mwitikio mkubwa wa Wananchi katika matembezi hayo (juu na chini).

Wananchi mbalimbali, wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu (juu na chini) wakipashapasha katika Viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya kutembea mwendo mrefu.

Kwaya ya Mahakama ya Tanzania ikitumbuiza katika hafla hiyo.

Related Posts